Showing posts with label WANASIASA. Show all posts
Showing posts with label WANASIASA. Show all posts

BUNGENI:MH ZITTO NA LEMA WAINGIA KATIKA VITA YA MANENO,CHANZO CHA MKASA HIKI HAP

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hali ya vurugu zinazoendelea Mtwara katika sakata la mradi Gesi asilia kuja Dar es Salaam.PICHA NA VENANCE NESTORY

Dodoma: Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii.
Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa.
Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye.
Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akisema:
“Mimi sikumtaja mtu, kwahiyo kama kuna mtu analalamika hilo ni suala jingine, ila mimi nilimaanisha nilichokisema”.
Hata hivyo, Zitto alieleza kuwa msimamo wa Lema ulikuwa unapingana na wabunge wengine wa Chadema, ambao waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.
Zitto alisema kuwa yeye mwenyewe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika waliwahi kupendekeza kuwa posho zifutwe.
“Mimi sipokei posho kabisa, posho za vikao na ndiye mbunge pekee ambaye hapokei posho ya vikao tangu mwaka 2011,” aliongeza Zitto, ambaye anahudhuria mkutano unaozungumzia uendeshaji wa Serikali kwa uwazi huko London, Uingereza.
Zitto alisema malipo ya wabunge mpaka sasa ni makubwa sana ukilinganisha na hali ya wananchi wakati Serikali ikishindwa kulipa vizuri walimu na wauguzi.
“Hatuwezi sisi kama wabunge kuanza kulilia posho, wakati wananchi wetu hawana maji, hatuwezi kulilia posho. Mbunge anayetaka posho zaidi akafanye kazi nyingine na awaachie wanaoweza kuwakilisha watu waendelee,” alisema Zitto.
Lema, hata hivyo, alisema kwamba katika mkutano huo aliweka bayana kwamba umasikini siyo uzalendo na kusisitiza kuwa wabunge wanapaswa kuwa na maslahi bora na wakati huohuo wana wajibu wa kuwatetea watumishi wengine wa umma.
“Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni haki wabunge kulipwa vizuri na wakati huo wapiganie maslahi ya watumishi wengine,” alisema Lema na kuongeza:
“Kwahiyo nikasisitiza kwamba nawashangaa wale ambao wanakataa posho ya Sh80,000 na ukienda kuchunguza wanakatwa fedha zote kutokana na mikopo waliyochukua, lakini bado wakija sehemu kama Arusha wanalala kwenye hoteli ya gharama kubwa kati ya Dola za Marekani 150 na 600”.
Alisema katika mazingira hayo kunakuwapo maswali mengi yasiyokuwa na majibu na kwamba mbunge wa aina hiyo alitakiwa anapokuwa katika mji wowote nchini aishi katika hoteli yenye thamani kati ya Sh20,000, 30,000 na hata Sh50,000.
“Kwa hiyo ikiwa unakataa posho ya Sh80,000 halafu unalala chumba cha Dola 600 hustahili kupata credibility (sifa) stahili, ni unafiki tu na kutafuta sifa za kipuuzi,”alisema Lema.
Alisisitiza kwamba wabunge wa Tanzania hawalipwi ipasavyo na kwamba kudai malipo ya ziada hakuwaondolei wajibu wao wa kuwatetea watumishi wengine wa umma ambao pia malipo yao ni kidogo.
“Kuna hatari ya kuona kwamba Sh80,000 au Sh200,000 ni fedha nyingi, ni kwamba kama sisi wabunge tutalipwa Sh50,000 basi maana yake ni kwamba walimu au polisi tutaridhika wakilipwa hata Sh10,000,”alisema
Mwananchi

VIGOGO WA CCM WALIOBAHATIKA KUPATA SHAHADA CHUO KIKUU HURIA,HAWA HAPA

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Makao Makuu, Daniel Chongolo, akipongezana na Mjumbe wa NEC ya CCM, Asha Abdallah Juma baada ya wote kutuniwa shahada zao katika mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika jana, Oktoba 27, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Chongolo ametunukiwa shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma na Asha shahada ya Pili ya Biashara. Katikati ni Kada wa CCM, Rachel Kyala ambaye pia ametunukiwa shahada ya Mawasiliano ya umma.(Picha na Bashir Nkoromo)
2_a76fe.jpg
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk. Asha-Rose Migiro, akimpongeza Kada wa CCM, Asha Abdallah Juma, baada ya kumtunuku shahada ya pili ya Biashara, katika mahafali ya 25 ya chuo hicho, yaliyofanyika jana, Oktoba 27, 2013, Makao Makuu ya OUT, Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Kushoto ni Makamnu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette. Asha ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC CCM, amewahi kuwa Waziri katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Katibu wa NEC, Oganaizesheni.

WABUNGE WATAKA KULIPWA KIINUA MGONGO BAADA YA KAMPENI ZA KUWANIA WADHIFA HUO! ,KISA CHA KAULI HIYO HIKI HAPA

KAULI ya Spika Anne Makinda, kwamba hali za wabunge huwa mbaya baada ya ubunge kukoma, imeonesha kuwauma baadhi yao ambao wamekiri kwamba ina ukweli. Baadhi ya wabunge hao wamefikia hatua ya kupendekeza wasilipwe kiinua mgongo, mpaka wamalize kampeni za kuwania kiti hicho baada ya muda wao kuisha, ili wasipochaguliwa, kiwasaidie kusogeza maisha mbele.
Wakizungumza na gazeti hili Ofisi Ndogo ya Bunge jana, baadhi yao walisema siasa ni jambo la ajabu, kwani aingiapo mtu hawezi kusema unaacha kugombea, ni sawa na kuathirika na jambo fulani kama vile mtumia dawa za kulevya.
“Ukiingia kwenye siasa, huwezi kusema unatoka, unakuwa mlevi sawa na mtumia dawa za kulevya, huwezi kuacha ndio maana hata sisi wabunge hatuwezi kuacha kugombea,” alisema Mbunge wa Bukene, Selemani Zedi (CCM) alipozungumza na gazeti hili katika ofisi ndogo za Bunge jana.
Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (CCM), alisema awamu ya ubunge inapokoma, hupewa Sh milioni 60 kama kiinua mgongo na kudai kuwa fedha hizo sio nyingi kwa kuwa hutumiwa kuendesha kampeni katika uchaguzi.
“Kiinua mgongo sio kikubwa, kinatofautiana na awamu, mfano mwaka 2010 ilikuwa Sh milioni 60, sasa unapewa wakati ndio unakwenda kwenye kampeni, unakuta unazitumia zote, halafu unakosa ubunge, hapo ndio dhiki zinaanza,” alisema Kawawa.
Alimshukuru Spika Makinda kwa kulisema hilo kwani maisha baada ya ubunge huwa magumu kwa kuwa hawana pensheni na kama Mbunge hana biashara au shughuli za kilimo, maisha ndio hapo yanaanza kudorora. Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk Muhammed (CUF), alisema hali ya wabunge wengi mara baada ya ubunge kukoma ni mbaya, kwa kuwa fedha wanazopata wakiwa wabunge, huzitumia na wananchi katika majimbo yao.
“Tunaomba utaratibu wa kupewa pensheni uwepo, hali sio nzuri kwa wabunge mara baada ya ubunge kukoma, kwa kuwa fedha tunazopata tunazitmia na wananchi kwenye kazi za maendeleo ya jimbo,” alisema Mbarouk.
Kawawa naye alisema tofauti na ilivyo katika mtazamo wa wananchi kwamba wabunge wana fedha nyingi, lakini hawana fedha na kidogo wakipatacho mara nyingi hukitumia kwenye majimbo yao, wakiamini uchaguzi mwingine ukija watachaguliwa.
Akizungumzia Mfuko wa Jimbo, Kawawa alisema fedha za Mfumo wa Jimbo sio nyingi kama wananchi wanavyodhani na kwamba zinatumika kwenye miradi katika majimbo husika, na wakati mwingine wanaingia mifukoni mwao kutoa fedha za miradi ya wananchi au kusaidia wananchi.
“Inafika mahali tunasahau hata familia, wake au waume zetu… tunapeleka fedha majimboni kusaidia wananchi. Wengine wanakulilia mpaka ada za watoto na mambo mengine,” alisema Kawawa.
“Mfano jimboni kwangu mfuko wa jimbo nimepata Sh milioni 47, nina kata 16, hivyo kila kata ninaipa Sh milioni tatu, hebu niambie zitajenga mradi gani kama sio mbunge kuingia mfukoni na kusaidia?” Alihoji Zedi.
Mbarouk (CUF), alikwenda mbali na kusema Spika amefikia kutamani wabunge wawe wajasiriamali, kutokana na utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa halmashauri wanaofuja fedha za umma na kushindwa kufikia malengo.
“Haiwezekani sisi tuonekane tumechoka hoi mpaka Spika wetu anafikiria kutusaidia tuwe wajasiriamali kwa sababu ya uzembe wenu. (Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wanaodaiwa kupoteza Sh milioni 273 zilizolekezwa kwa matumizi ya shughuli za maendeleo katika halmashauri hiyo.)
“Tunaonekana tumechoka kwa kuwaza majibu kwa wananchi ya mambo ambayo fedha imetengwa baada ya kuyapigia kelele na kupitisha bajeti bungeni, kwa kweli tutabanana mpaka kieleweke,” alisema Mbarouk.

WANASIASA WALIOHOJIWA KWA KUWA NA MALI NYINFI NJE YA NCHI HAWA HAPA,ILIKUA HIVI...

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja na Mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, wamehojiwa kuhusu kuwa na utajiri mkubwa nje ya nchi.
Wanasiasa hao wamehojiwa na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na serikali hivi karibuni kwa ajili ya kutafuta mali mbalimbali zilizofichwa nje ya nchi na watu mbalimbai wenye nyadhifa kubwa.
Ingawa watendaji wakuu wa kikosi kazi hicho wamekataa kuthibitisha au kukana kuhusu kuhojiwa kwa wanasiasa hao, Raia Mwema limeambiwa wanasiasa hao ni sehemu tu ya watu zaidi ya 100 wanaochunguzwa na vyombo vya dola.(P.T)
Kikosi hicho kiliundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kinaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah na wawakilishi kutoka Jeshi la Polisi, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na waatalamu wa masuala ya kibenki.
Chanzo cha kuaminika cha kilisema Mbowe ambaye pia ndiye Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alihojiwa kutokana na maelezo kuwa alinunua jumba la kifahari nchini Dubai, Desemba mwaka 2011.
"Kutokana na wadhifa wake kwa umma, Mbowe ilibidi achunguzwe kutokana na ununuzi wa nyumba alioufanya nchini Dubai, Desemba mwaka 2011.
Uchunguzi wake ni mahususi kwa sababu tumefuatilia akaunti zake na ikaonekana hakuwahi kutumia njia ya benki kufanya malipo.
"Hii maana yake ni kwamba kama alifanya malipo, basi alifanya kwa kutumia fedha taslim (cash).
Sasa ni lazima ichunguzwe maana si kawaida kwa kiongozi kama yeye kusafiri na mamilioni yote ya kununua jumba kule Dubai na kulipa cash. Ndiyo maana yeye anafanyiwa uchunguzi mahususi," kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili.
Rostam ni miongoni mwa wafanyabiashara maarufu hapa nchini na Raia Mwema limeelezwa kwamba alihojiwa kutokana na kumiliki jumba katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati na imeelezwa pia kuwa ana akaunti kadhaa nje ya nchi.
Dubai ni kimbilio la wafanyabiashara wengi kutokana na nafuu ya kodi inayotolewa na serikali ya nchi hiyo na pia uwepo wa biashara na usalama mkubwa uliopo.
Zaidi ya kuwa mfanyabiashara maarufu, Rostam aliwahi kuwa mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alipata pia kuwa Mweka Hazina wa chama hicho.
Hadi tunakwenda mitamboni, gazeti hili lilikuwa halijafahamu ni kwa sababu ya mali zipi hasa ambazo Ngeleja anazo lakini wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini, kulikuwa na minong'ono kwamba alikuwa miongoni mwa mawaziri vijana wenye ukwasi mkubwa alioukwaa ndani ya muda mfupi.
Alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu alichohojiwa alipoitwa na kikosi kazi, Ngeleja alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi; "Samahani, mimi si msemaji wa suala hilo." Hata alipoombwa na mwandishi walau kukanusha au kukataa kuwa alihojiwa – Ngeleja alijibu kwa ufupi, "Ahsante."
Kwa sasa, waziri huyo wa zamani wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete yuko safarini nje ya nchi.
Alipotafutwa wiki hii kueleza upande wake kuhusu alichohojiwa, Rostam hakujibu simu wala ujumbe mfupi wa maneno aliotumiwa na mwandishi.
Mbowe hakuwa tayari kueleza kuhusu kuhojiwa huko ingawa Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, aliyeeleza kuwa ameagizwa kujibu kwa niaba ya mkuu huyo wa upinzani, alisema; "si jambo la ajabu kwa Mbowe kuwa na mali nje ya nchi kwa vile ni mfanyabiashara na ana biashara hadi nje ya nchi."
Kikosi kazi kinafanya kazi zake katika mazingira ya usiri na tangu kilipoanza kazi mapema mwaka huu, hakijawahi kutoa taarifa rasmi kuhusu shughuli zake.
Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho, Dk. Hoseah alikataa kuzungumza chochote kuhusu watu waliowahoji kwa maelezo kuwa msemaji wa shughuli yao ni Werema.
Werema hakutaka kukana wala kuthibitisha taarifa hii isipokuwa katika mazungumzo ya nyuma na vyombo vya habari aliwahi kusema kwamba ni kinyume cha maadili kwa tume hiyo kutoa taarifa kuhusu watu iliowahoji.
Novemba mwaka jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, alitoa hoja binafsi bungeni akitaka ufanyike uchunguzi wa fedha na mali haramu kutoka Tanzania zilizofichwa katika nchimbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, raia wake hawaruhusiwi kufungua akaunti katika nchi za kigeni pasipo ruhusa ya ofisi ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
Katika hoja yake binafsi, Zitto alitaka Bunge lipewe nguvu ya kuunda Kamati Teule ambayo itachunguza na kubaini ni akina nani wanamiliki akaunti na mali ughaibuni lakini serikali iliamua yenyewe kuwa ndiyo itafuatilia kwa kutumia vyombo vyake.

MAKUBWA:WABUNGE WASTAAFU WALIA NJAA KWA SPKA, TAZAMA ILIVYOKUA

Spika wa Bunge, Anne Makinda.
OFISI ya Bunge inaangalia utaratibu wa kufundisha wabunge ujasiriamali baada ya kubainika baadhi ya wanaokoma kushika wadhifa huo, kukabiliwa na hali mbaya ya ukwasi na kulazimika kuomba msaada.
Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema maisha ya siasa kwa sasa sio kazi ya kutegemea kwa sababu hawana mkataba na wananchi; hivyo umefika wakati kuangalia jinsi ya kufundisha wabunge ujasiriamali kuondokana na adha ya ukata mara ubunge unapokoma.
Akizungumza na Spika wa Bunge la Uswisi, Maya Graf jijini Dar es Salaam jana, Spika Makinda alisema moja ya changamoto inayokabili bunge hivi sasa ni kwamba wabunge hawana pensheni baada ya ubunge kukoma. Alisema baadhi ya wabunge wamekuwa katika hali mbaya kifedha mara wamalizapo kipindi chao cha ubunge.
“Kwa kweli hali ni mbaya, ni wakati sasa umefika tutaanzisha programu ya kuwafundisha ujasiriamali wabunge, ili wawe na kitu cha ziada cha kufanya, ili hata kama hatachaguliwa kwenye awamu nyingine, asiwe kwenye hali mbaya kimaisha, awe na kitu cha kufanya”, alisema Makinda.
Akifafanua hilo alisema siasa siyo kazi ya kudumu kwa sasa, na kwamba hata wale wanaokosa nafasi ya kurudi bungeni kwa awamu nyingine, huwa vigumu kupata ajira kwa kuwa hata waajiri hudai hao ni wanasiasa.
Alisema, ubunge ni kazi ambayo mtu anakuwa na mkataba na wananchi na kwamba kama wananchi wataamua kutomchagua kwa mara nyingine, ndio mwisho wa ubunge hivyo ni vyema kuwa na kazi mbadala kufanya maisha yaendelee.
Alisema ingawa ubunge ni kazi ambayo haina pensheni baada ya mhusika kumaliza kipindi , lakini wanapokuwa kwenye nafasi, fedha wanazopata huzitumia pia kwa ajili ya maendeleo ya majimbo yao.
Mishahara ya wabunge Aidha, alisema ingawa mishahara ya wabunge siyo mikubwa kama ilivyo kwa wabunge wa nchi nyingine, hata kama ikiongezwa haitatosha kutatua matatizo wanayokumbana nayo.
“Wakipatacho mara nyingine hukitumia pia kwenye majimbo yao kusaidia wananchi,” alisema.
Aliongeza, “Kwa kweli tuna changamoto, nafasi ya ubunge haina pensheni mara ubunge unapokoma, tunapata kiinua mgongo, sasa kama mbunge hakuchaguliwa tena kuendelea na nafasi hiyo, kwa awamu nyingine baadhi yao wanakuwa kwenye hali mbaya.” Waomba mshiko Aliongeza,
“hali ni mbaya, wapo wabunge wastaafu unawaona unashituka, wengine wanafululiza hapa unawapa chochote ulichonacho sasa, ili kuondokana na adha hii tunaangalia jinsi ya kuwasaidia kabla ya kumaliza kipindi cha ubunge wawe na kazi au biashara”.
Hata hivyo alisema hivi sasa wabunge wengi ni vijana na kwamba kwa hali halisi ya kazi ya ubunge ni wazi kwamba wenye uamuzi ni wananchi, hivyo ikiwa wanakosa kwa awamu nyingine, na hawana kazi nyingine ya kufanya, hali itakuwa mbaya zaidi.
Akifafanua jinsi watakavyoweza kugawa muda wa ujasiriamali na kazi ya ubunge, Makinda alisema katika programu hiyo wataangalia pia jinsi ya kutenga muda ili kufanya mambo yote kwa ufasaha na umakini. Rafu katika uchaguzi
Akizungumzia uchaguzi Makinda alisema, chaguzi nyingi za ubunge zimekuwa za kufa kupona kwa wagombea kwa kuwa wanafahamu ikiwa watakosa na hawana kazi nyingine, huo unakuwa mwanzo mgumu wa maisha.
“Mnapogombea nafasi ya ubunge kwenye majimbo ya uchaguzi unakuwa wa kufa au kupona kwa kuwa wengi wa wagombea wameacha kazi au hawana kazi na kama watakosa nafasi hiyo basi hapo ndio ugumu wa maisha unaanza”, alisema Makinda.
Kadhalika, alisema ili kuondoa migongano na ugomvi mara baada ya uchaguzi kumalizika, ni vyema wabunge wakafundishwa ujasiriamali ili kama akiwania nafasi na kushindwa kwa haki asiwe na kinyongo na aliyeshinda, bali atafanya biashara kwa kuwa ana elimu au mafunzo.
Spika wa Uswisi ashauri Kwa upande wake Spika wa Uswisi, Maya Graf alisema mfumo wa Bunge la Tanzania na wa kwao hautofautiani kwani wao pia kama mbunge hatachaguliwa kwa awamu nyingine, hufanya kazi nyingine.
“Kwetu kupata kazi sio shida, ukiwania nafasi ya ubunge ukakosa, unaweza kupata kazi kwa kuangalia fani uliyonayo, hii ndio tofauti ya kwenu na kwetu, ila kupata ubunge ni matakwa ya wananchi kama wanakukubali”, alisema Graf.
Aliongeza kuwa ni vyema changamoto hiyo ya ajira au biashara mara baada ya ubunge kukoma ikaangaliwa na kutafutiwa ufumbuzi, ili kuwasaidia wabunge waweze kuendelea na maisha na kuondokana na umaskini.

CHANZO HABARI LEO

KAMATI YA ZITO KABWE,YADAIWA KUITENGA CUF,MSIMAMO WA KAFU UNASEMA HIVI....


*Wasema hata ikiwaita hawatakwenda kuhojiwa
*Chadema, NCCR-Mageuzi wapigilia msumari 
HOJA ya ukaguzi wa ruzuku za vyama vya siasa iliyoibuliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, imeendelea kuvivuruga vyama vya siasa.

Baadhi ya vyama vilivyotajwa na kamati hiyo vikidaiwa kushindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa ruzuku kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, vimetoa misimamo yao inayoonyesha kutokukubaliana na kauli ya Zitto.

CUF kwa upande wake, kimetishia kwenda mahakamani endapo msajili ataamua kusimamisha ruzuku kama alivyoagizwa na Zitto kwa kile walichosema kuwa hakuna sababu za msingi chama chao kutopewa fedha hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema hawana wasiwasi na hesabu zao na kama msajili ataamua kuisimamisha, watakwenda mahakamani.

Alisema msajili wa vyama vya siasa hawezi kufuta ruzuku ya chama chao wakati wanao ushahidi wa nyaraka zinazothibitisha ofisi yake ilipokea hesabu zao zilizokaguliwa.

Mtatiro alisema kuwa, hesabu ambazo wao hawajapeleka kwa msajili ni za mwaka 2012/2013 na si miaka minne kama Zitto alivyosema. Kutokana na hali hiyo, alisema kuna uwezekano msajili aliyemaliza muda wake hawakukabidhiana baadhi ya nyaraka ndiyo maana inasemekana ukaguzi wa hesabu zao hauko vizuri.

“Sisi hatufanyi kazi na Kamati ya Zitto isipokuwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye anapaswa kuhojiwa kama kuna upungufu katika jambo lolote,” alisema Mtatiro.

Kiongozi huyo wa CUF alisema kwamba, awali walikuwa wakifanya ukaguzi wao wa ndani na kupeleka hesabu kwa msajili, lakini mabadiliko yaliyowataka kumlipa mkaguzi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ndiyo yaliyowatia shaka.

Pamoja na hayo, alisema chama chake hakitakwenda mbele ya Kamati ya Zitto kujieleza, kwani hakiwajibiki kwao.

“CUF si Serikali, si utaratibu wala sheria kwa vyama vya siasa kutafuta mkaguzi wake binafsi, mtu hawezi kujikagua mwenyewe badala yake tutasababisha mgongano wa kimaslahi, hii ni aibu kwa Serikali kutokuwa na wakaguzi.

“Ingawa tunatambua Kamati ya Bunge ina uwezo wa kumwita mtu yeyote, tunasema hatutakwenda kwenye kamati hiyo japokuwa hatujapata wito rasmi na tunamtaka Zitto aache kutuchafua kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Mtatiro.

MARA.DIWANI WA CHADEMA APIGWA NA KUJERUHIWA VIBAYA


WATU sita wamelazwa katika Hospitali ya DDH-Bunda, mkoani Mara, kutokana na kujeruhiwa vibaya kwa kile kinachodaiwa ni kupigwa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambao wanaendesha operesheni ya kusaka wawindaji haramu.
Mganga Mkuu katika wodi ya wanaume hospitalini hapo, Dk. Alphonce Kwessi, alisema kuwa majeruhi waliopokewa hospitalini hapo ni pamoja na Diwani wa Kata ya Nyarikoba wilayani Tarime, Mustapha Mashani, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye  ameruhusiwa baada ya hali yake kutengamaa.
Dk. Kwessi alisema kuwa majeruhi wengine ambao bado wamelazwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipaso wilayani Tarime, Robert Mrenda (CCM), Saguda Mihayo, Makoye Kazi, Ezekiel Nyarusi na Igeye Wambura.
Alisema kuwa majeruhi hao wamefikishwa hospitalini hapo tangu Oktoba 16, mwaka huu wakiwa na hali mbaya na kwamba waliletwa na askari hao pamoja askari wa Tanapa, wakidai kuwa wamekamatwa kwa tuhuma ya uwindaji haramu.
Hata hivyo diwani huyo wa CHADEMA juzi alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda na kushitakiwa kwa uwindaji haramu, ambapo alipatiwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kutokana na suala hilo, Mratibu wa Mafunzo Kanda ya Ziwa Mashariki wa CHADEMA, Chacha Heche,  juzi alifika hospitalini hapo, alisema chama chao hakiridhiki kabisa na nguvu kubwa iliyotumika katika kuwakamata watu hao.
Heche alisema kuwa wapo watu waliokamatwa bila kuwa na vielelezo wakati wakiwa majumbani mwao, akiwamo diwani huyo.
“Haturidhishwi na nguvu kubwa iliyotumika na mamlaka inayofanya kazi ya kusaka wawindaji haramu kiasi cha kukiuka na kuvunja miiko na taratibu za haki za binadamu,” alisema.
Alisema kuwa wao kimsingi hawapingi zoezi hilo la kukamata wawindaji haramu lakini inabidi liangaliwe upya, kwani nguvu inayotumika katika kukamata watuhumiwa ni kubwa mno, ikiwa ni pamoja na watuhumiwa kupewa adhabu za kijeshi.
“Huu ni ukiukwaji mkubwa  wa haki za binadamu, watu wamekamatwa bila kuwa na vielelezo, tena wengine majumbani mwao, kwa mfano diwani huyu, lakini baada ya kukamatwa walifichwa kwenye kambi mbalimbali, wamepigwa sana, yaani ukiwaona utashangaa, wamesema eti walikuwa wanapewa adhabu za kijeshi,” alisema.
Polisi wilayani Bunda walithibitisha kuwapo kwa majeruhi hao, hawakuwa tayari kutoa taarifa zaidi kwa madai kuwa ni operesheni ya kitaifa.
SOURCE .TANZANIA DAIMA

CHANZO CHA AJALI ILIYOKATISHA UHAI WA DADA WA MBOWE HIKI HAPA...........

Majeruhi wa ajali hiyo, Zedii Mzuke  na mtoto wake wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe kwa matibabu.
Familia ya Mwenyekiti Chadema Taifa, Freeman Mbowe, imepata pigo baada ya dada wa mwenyekiti huyo, Grace Mbowe, kufariki katika ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokea jana   katika eneo la Changa Kabuku, barabara ya Segera-Chalinze, ambapo gari lenye namba za usajili T 277 CAT aina ya Toyota Crester Saloon Gx 100, likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam, liliacha njia na kupinduka.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, gari hilo lilikuwa limebeba watu watano, akiwemo Grace Mbowe na dereva aliyetambulika kwa jina la Ibrahim Mkindwa. 
Mashuhuda hao walidai chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari, uliosababisha tairi la nyuma upande wa kulia kupasuka. Hali  hiyo ilisababisha dereva kushindwa kumudu kona, hivyo kusababisha kupinduka na kuingia chini ya daraja.
Katibu wa Mbunge Mbowe, Richard Mtui, alithibitisha kutokea kwa msiba huo na kuongeza kuwa Chadema Hai imesitisha mikutano ya hadhara, kusubiri taratibu zingine.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa bado Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi.
Massawe alitaja majeruhi watatu waliokuwa abiria katika gari hilo kuwa ni Ridhiwani Bakari (29), Zedii Mzuke (28) na mtoto  Mariam Ridhiwani (3), wote wafanyabiashara wa Msambweni mkoani Tanga.
Alisema miili ya marehemu na majeruhi, walipelekwa katika Hospitali ya Magunga Korogwe mkoani Tanga.
Kifo cha dada yake na Mbowe, kimetokea ikiwa ni siku chache  baada ya kuhama Chadema na kujiunga na  CCM.

MH ZITTO KABWE AWASILISHA BARUA KWA KATIBU WA BUNGE INASEMA HIVI.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRCxBtynXOdrR-HnnZvPh-aG80__w3Q3-juBCZ6m31tcKDMIHt7Md1jRXOZLzGK96vZuQwD2ymWQXG3q5aMpM2bM7L4gpDn0EnNMLWRYWOveOOAf6YOjYH8W_SnTSMn3r571TslaSNiBAI/s640/Zitto-Kabwe.jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Bw.Zitto Kabwe(CHADEM A),ameandika barua kwenda kwa Katibu wa Bunge akimkumbusha azimio la Bunge namba 9/2012 kuhusu Watanzania walioficha fedha nje ya nchi.
Katika barua hiyo,Bw.Zitt oalisema Mkutano wa Tisa wa Bunge la 10 uliofanyika mwezi Novemba 2012,kutokana na hoja binafsi ya mbunge,Bunge lil ipitisha Azimio la Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma za Watanzania kuficha mabilioni ya fedha za kigeni katika Benki za Ughaibuni hasa nchini Uswisi.Alisema Bunge liliagiza taarifa ya utekelezaji wa Azimio hilo iwe imewasilishwa bungeni kwenye Mkutano wa 11(Aprili,2013).Kutokana na kubadilishwa mfumo wa Bajeti ya Nchi,mkutano huo ulikuwa wa bajeti hivyo ilitaraji wa taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa azimio hilo,ingewasilishwa bungeni katika mkutano wa Agosti-Septemba 2013 lakini ilishindikana. " Pamoja na kwamba hoja ikishaamuliwa na Bunge ni hoja ya Bunge si ya mtoa hoja tena...nikiwa mdau mkubwa kwenye hoja hii, napata mashaka kwa nini Serikali imeshindwa kuwasilisha taarifa bungeni kwa mujibu wa Azimio la Bunge. "Kutowasilishwa taarifa hii,kunaleta wasiwasi miongoni mwa wananchi kuwa hoja husika imetupwa kapuni na Taifa halitapata ukweli kuhusu utoroshaji wa fedha za kigeni nje na kufichwa katika benki au kununua mali ughaibuni kama majumba,"alisema.Bw. Zitto aliliomba Bunge liitake Serikali iwa silishe taarifa hiyo juu ya utekelezaji wa Azimio la Bunge namba 9/2012 kuhusu Watanzania walioficha mabilioni nje kwenye mkutano wa Bunge uliopangwa kuanza Oktoba 29, mwaka huu
-majira

WAZIRI CHIKAWE AMTISHA JK: AMWOMMBA ASAINI MUSWADA KUEPUSHA FURUGU...

 Wenyeviti wa vyama vya Upinzani,Freeman Mbowe wa Chadema(Kulia) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF(wapili kulia)wakiagana na viongozi wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu jijini Dar es Salaam jana baada ya mazungumzo kuhusu kupinga Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, atamshangaa Rais Kikwete ikiwa atasikiliza kelele za wapinzani kwa sababu walishirikishwa kupitia kamati na hata bungeni kabla ya kupitishwa kwake.
“Nitamshangaa sana Rais Kikwete kama atashindwa kusaini muswada huo kwa sababu ya kelele za wapinzani. Tuliwashirikisha katika kila mchakato kabla na baada ya kuuwasilisha bungeni,” alisema Chikawe.
Alisema kitendo cha wapinzani hao kujiunga pamoja na kuanzisha kampeni za kuwahamasisha wananchi ili waukatae muswada hakisaidii lolote, kwa sababu sheria zote zinatungwa bungeni na siyo kwenye Viwanja vya Jangwani wala Ikulu.
Vyama vyampinga JK
Wakati Chikawe akisema hayo, viongozi wa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi wameshikilia msimamo wao kwamba wataendelea kupinga muswada huo uliopitishwa na Bunge, Septemba 6, mwaka huu.
Wakizungumza Dar es Salaam jana walipokutana na Shura ya Maimamu ikiwa ni mwendelezo wao wa kukutana na asasi za kiraia, viongozi wakuu wa vyama hivyo, walisema kamwe kasi yao ya kutaka kutosainiwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haiwezi kupunguzwa kwa namna yoyote kwa kuwa wanatetea masilahi ya Watanzania na siyo mtu binafsi.
Kauli yao imekuja siku moja baada ya Rais Kikwete kusema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakisema uongo kuhusu mchakato wa Katiba unavyokwenda.
Wanasiasa pia hao wamepinga matumizi ya kauli za kibabe kwenye mchakato huo na kuonya kuwa nguvu ya dola haiwezi kushindana na nguvu ya umma.
Mbali na hayo, wanasiasa hao walisisitiza kwamba hawatapiga magoti kuomba Katiba Mpya, kwani ni ya Watanzania wote na si mali ya wanasiasa, chama cha siasa wala wabunge.
Rais Kikwete alikaririwa na magazeti mbalimbali jana akipinga madai ya wapinzani kuwa hakuzingatia maoni yao wakati wa uteuzi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Nafahamu kwamba tunaambiwa tunasema uongo, lakini ni vizuri ifahamike wazi kuwa hatuwezi kupunguzwa nguvu na kauli hizo alizozitoa Rais Kikwete, kwani msimamo tulionao ni kuendelea kutetea Watanzania,” alisema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbowe alimshauri Rais Kikwete atumie busara kwa kutosaini mkataba huo ili mchakato uende vizuri.
-mwananchi

RAIS KIKWETE AWASHUKIA WANASIASA ...

 


Rais Jakaya Kikwete
*Asema hatawatetea wauza ‘unga’
*Ashangazwa na kiwango cha uongo

RAIS Jakaya Kikwete, amesema anashangazwa na kiwango cha uongo cha baadhi ya wanasiasa ambao hakuwataja majina, kuwa wamekuwa wakizusha madai kuwa Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbalimbali waliopendekeza majina hayo.
Alisema bado anaendelea kuamini mchakato wa Katiba mpya utafikia mwisho wake mwaka 2014 na hivyo kuiwezesha Tanzania kufanya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, chini ya Katiba mpya.

Alisema hana tatizo na watu wanaopinga sera za serikali ama hata kumpinga yeye binafsi, bali tatizo lake ni wanasiasa na wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.

Rais Kikwete, aliyasema hayo juzi, mjini San Rafael, California, nchini Marekani, wakati alipokutana na kuzungumza na jumuia ya Watanzania waishio katika Jimbo la California.

Katika hotuba yake, ambayo alizungumzia mambo mbalimbali, Rais Kikwete aligusia mjadala wa karibuni bungeni kuhusu mchakato wa Katiba mpya na kusema kuwa alishangazwa na madai kuwa yeye kama Rais, hakuongozwa na mapendekezo ya wadau wakati anateua Tume ya Katiba.

“Watu wote niliowateua walipendekezwa na wadau mbalimbali, zikiwamo taasisi za dini. Yule Mama Maria Kashonda alipendekezwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mama Mwantumu Malale alipendekeza na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA). Kila kundi ambalo lilipendekeza watu limepata mjumbe katika tume hiyo, wakiwemo walemavu ambao naambiwa nimewasahau,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:



Kuhusu kama Tanzania itaweza kupata Katiba mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Rais Kikwete alisema: “Ningependa sana na kwa kweli ni matarajio yangu makubwa, tuweze kumaliza mchakato wetu mwaka 2014 na tuweza kuwa na Katiba Mpya ili iongoze Uchaguzi Mkuu wetu wa mwaka 2015. Mchakato wetu unakwenda vizuri na wala siyo lazima tuhangaike na Katiba kwa miaka mingi. Muhimu ni ushirikishwaji wa kila mmoja wetu.”

Akizungumzia tabia za wanasiasa wa Tanzania kwa jumla, hasa wale wanaochochea chuki na ghasia, Rais Kikwete aliwaambia Watanzania hao:

“Sina tatizo na wanasiasa ama wanaharakati kupinga sera za Serikali yangu. Hili ni suala la nguvu ya hoja na tunao uwezo mkubwa sana wa kutetea sera zetu. Na wala sina tatizo na watu kunipinga mimi binafsi. Kinachonipa taabu mimi ni pale wanasiasa na wanaharakati wanapochochea ghasia na kuleta fujo. Kama mtu anataka kuongoza Tanzania si asubiri hadi atakapochaguliwa?”

Aliongeza Rais Kikwete: “Hivi unapochochea ghasia, fujo na chuki na kweli mambo hayo yakatokea na nchi ikateketea, utaongoza nchi ya namna gani? Utaongoza magofu na majivu yatakayobakia baada ya nchi kuteketea?”

Kuhusu mjadala wa karibuni kuhusu kama Rais awe na madaraka ya kuteua wajumbe 166 wa nyongeza ili kuingia katika Bunge la Katiba kujadili Rasimu ya Katiba Mpya, Rais Kikwete amesema kuwa yeye hana tabu kama itabidi ateua basi atateua, lakini kama siyo lazima yeye hana tabu.

MTANZANIA

MWANZA:WAZIRI WAGUFULI AZOMEWA MBELE YA RAIS KIKWETE .



RAIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.

Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.

Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.

Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza.

Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!

Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio.

Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.

Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power’.

Katika hatua ya kushangaza wananchi hao walimshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais huku wakiwazomea Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, ambaye hakufika kabisa mkutanoni hapo.

Matata alionekana mapema wakati Rais Kikwete akisomewa taarifa ya maendeleo makao makuu ya wilaya hiyo lakini hakufika uwanjani kabisa katika viti vya mbele alionekana naibu wake, Swila Dede.

Baadhi ya wananchi hao walisikika wakisema chini kwa chini kuwa Matata ni mwizi hawataki kumsikia lakini shangwe na nderemo zikajiri pale walipotambulishwa Wenje na Kiwia.

Rais Kikwete akiwa wilaya ya Ilemela, wananchi wengi waliokuwa wamesimama njiani walimwonyesha vidole viwili ikiwa ni alama CHADEMA.

Hata hivyo, hali hiyo ilionekana kumkera kiongozi huyo wa nchi pamoja na maofisa wa usalama, ambapo wana usalama wakiwemo polisi walionekana wakiwatisha na kuwazuia wananchi kunyoosha vidole viwili.

Magufuli azomewa
Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata, ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.

Adha Magufuli alizomewa pia aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM.

Pia aliendelea kuzomewa aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.

“Mheshimiwa Rais, nampongeza Meya Matata (akazomewa), lakini pia wabunge wa Ilemela na Nyamagana wanachapa kazi vizuri, nje CHADEMA lakini ndani wao CCM (akazomewa).”

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.

Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta,” alisema.

Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba. 

-Tanzania daima
 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved