Home » , , » UCHAWA WASADIKIWA KUWA CHANZO CHA AJALI NA VIFO KWA WAIMBAJI WA INJILI....HABARI KAILI IHAPA

UCHAWA WASADIKIWA KUWA CHANZO CHA AJALI NA VIFO KWA WAIMBAJI WA INJILI....HABARI KAILI IHAPA


Gladness Mallya na Chande Abdallah KUTOKANA na ajali na vifo kwa muziki wa Injili vilivyotokea hivi karibuni, imedaiwa kuwa baadhi vimetokana na uchawi.Baada ya kuzagaa kwa habari hizo, mapaparazi wetu walimtafuta Rais wa Chama cha Muziki wa Injili, Addo Novemba ambapo alikiri kuwa kweli uchawi upo na unahusika.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili, Addo Novemba.
“Kwenye msafara wa mamba hata kenge wapo, hili la uchawi silikatai kwani hata kwenye vitabu vya dini limetajwa, kwa hiyo watu wafahamu kwamba tuna vita kali.
“Hata mimi ninasikia kuna baadhi ya waimba Injili na wachungaji wanaoenda Nigeria kwa ajili ya kuchukua nguvu za kishirikina lakini tunaendelea kuomba tunaamini Mungu anatupigania,” alisema Addo.
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Baadhi ya waimbaji waliofariki hivi karibuni ni pamoja na Deborah John Said (Juni 20), Egla Bavuma (Julai 22), Orida Njole (Julai 12) na Mandilindi William (Julai 15). Waliopata ajali ni Edson Mwasabwite na Bahati Bukuku ambao wote wanaendelea vizuri na matibabu,

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved