Home » , » WANAUME:SABABU ZA KUTOKWA NA MANII WAKATI WA HAJA KUBWA HIZI HAPA

WANAUME:SABABU ZA KUTOKWA NA MANII WAKATI WA HAJA KUBWA HIZI HAPA


Ni Matumaini yangu kwamba wasomaji wangu mpo sawa na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Kwa mara nyingine tunakutana katika kona hii ambapo baada ya wiki iliyopita kujibu maswali yenu kwa uchache, leo tunaendelea na mada mpya.
Tutazungumzia tatizo linalowasumbua baadhi ya wanaume la kutokwa na manii (mbegu za kiume) wakati wa kujisaidia haja kubwa. Hali hii imekuwa ikiwasumbua wanaume na wavulana wengi ingawa ni wachache wanaojitokeza na kueleza kinachowasumbua.
Hali hii kitaalamu huitwa ‘ejaculation during bowel movement’ ambapo mwanaume hutokwa na manii bila mwenyewe kujijua au kuhisi hali yoyote wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Endapo hali hii inajitokeza mara chache, huwa haina tatizo kwani kinachotokea ni kwamba mtu anapochuchumaa, viungo vya uzazi hasa mfuko wa manii (epidydimis) hukandamizwa na misuli ya miguu, mapaja pamoja na ya kiuno hivyo kulazimisha kilichomo ndani yake (manii) kutoka.
Lakini endapo tatizo hili linajirudia mara kwa mara, likiambatana na maumivu kwenye uvungu wa viungo vya uzazi au katika njia ya mkojo huwa ni dalili ya magonjwa mengine ikiwemo saratani ya kibofu (prostate cancer) hivyo ni lazima mhusika awahi hospitalini kwa ajili ya vipimo kisha matibabu.
Angalizo: Endapo tatizo hili linajirudia mara kwa mara, usitumie dawa bila kuonana na daktari kwani unaweza kuongeza ukubwa wa tatizo.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved