Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa bomu la kwanza kurushwa kwenye Vita ya Kwanza ya Dunia (WWI) kwa upande wa Afrika Mashariki lilitupwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Bomu hilo lililokusudiwa kuharibu mfumo wa
mawasiliano bandarini, lilirushwa kutoka kwenye meli ya Waingereza
iliyojulikana kama Astrea siku ya nne tangu kuanza kwa vita hivyo
vilivyoua watu milioni 16 duniani kote.
Akizungumza nyumbani kwa Balozi wa Uingereza
nchini, jijini hapa juzi, wakati wa kuazimisha miaka 100 ya WWI Afrika
Mashariki, Mratibu wa Taasisi ya Great War in Africa, Dk Anne Samson
alisema kuwa baadhi ya watu hawafahamu kuwa harakati za vita hivyo
zilifanyika Tanganyika.
“Dar es Salaam ilipigwa bomu kutoka baharini
Agosti 8, 1914 na wiki moja baadaye, Agosti 15, 1914 Jeshi la Ujerumani
likiwa na askari 200 liliivamia Kenya katika mpaka wa Holili na Taveta
wakati huo ikitawaliwa na Uingereza.