Hakuna
ubishi Cristiano Ronaldo ni moto uwanjani na anatajwa kama mmoja ya
wachezaji bora wa dunia. Hivyo mchezaji bora wa dunia mtu ambaye ni
nembo ya soka, hivyo anahitaji kuwa vitu bora kimojawapo ni mwanamke,
huyu hapa mtoto wa kirusi anaitwa Irina Shyk ni kweli kabisa anastahili
kuwa demu wa mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo. Irina Shyk ndio
anatufungia listi yetu ya wasichana ambao wana mvuto wamewahi ama wapo
katika mahusiano na wanasoka.
Antonella
Ruccozzo, binti wa kiaregentina ndiye aliuteka moyo wa mwanadamu ambaye
inasemekana yupo tofauti na wacheza soka wote kwa uwezo wake wa
kulisakata kabumbu. Huyu mtoto ni ndiye usingizi wa Lionel Messi -
mchezaji bora wa dunia kwa sasa.
Anaitwa
Aida Yespica, alikuwa galfriend wa mcheza soka Matteo Ferrari ambaye
alizaa nae mtoto. Kwa sasa huu ni usiungizi wa moja ya viiungo bora
duniani Mesut Ozil wa Real Madrid.
Ana
mtoto mmoja na moja ya kiungo bora wa ulinzi kuwahi kutokea katika soka
la karibuni Claude Makelele. Anaitwa Noemie Lenoir, unaambiwa si tu
Makelel alikuwa anajua kuzuia mashambulizi ya uwanjani tu kwani huko
Ufaransa mtoto anatingisha hatari lakini Makelele anawatuliza mapedeshee
wote wanaomsumbua mama watoto wake.
Mke wa mchezaji wa Tottenham Hotspur Rafael Van Der Vaart ni hatari. Anaitwa Sylivie Van Der Vaart.
Moja kati wengi waliotekwa na mtoto wa Kireno Cristiano Ronaldo. Letizia Filippi moja ya washiriki wa Miss Italy mwaka 2007.
Anajulikana kama ex-wife wa Ashley Cole - Cherly Tweedy aka Cherly Cole. Muimbaji na mwandishi wa nyimbo wa kiingereza.
Anaujua
uwendazimu wote hata ambao kijana Wayne Rooney hatuoneshi uwanjani.
Muite Coleen Rooney aka Mama Kai. Mwanamke wa kwanza katika maisha ya
Rooney na ndio anayejua kumtuliza Rooney kuliko hata babu Fergie.
English actress amekuwa na mahusiano na wanasoka kadhaa. Alianza na Cristiano Ronaldo, na baadae akachumbiwa na Marcus Bent.
Iker
Cassilas hajui tu kudaka mipira pia ana uwezo mkubwa wa kuwakamata
watoto wazuri. Huyu Eva Gonzalez nae aliwahi kumpitia katika kipindi
cha fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Alipigiwa
kura kuwa"Mtangazaji mwenye mvuto kuliko wote na jarida la FHM,
Carbonero anafahamika kwa tabia yake ya kupenda kumkiss in public
boyfriend wake Iker Cassilas, katika kila mechi ya World Cup 2010. Pia
katika fainali hizo alishutumiwa kwa kumkosesha umakini Cassilas katika
mechi waliyofungwa na Uswiss. Mmmmh mtoto alivyo mzuri hivi mie hata
simlaumu Cassilas.
Mwigizaji
wa kike maarufu kwa TV Series maarufu duniani kwa sasa iitwayo NIKITA.
Anaitwa Maggie Q demu wa zamani wa mchezaji bora wa Asia Hidetoshi
Nakata.
Model
huyu wa kibrazil pia yeye mwenyewe aliwahi kuwa mwanasoka. Yumo katika
listi hii kwa sababu ya aliwahi kuolewa na mwanasoka bora wa dunia mara 3
Ronaldo De Lima na wana mtoto mmoja. Pia sasa ameolewa na mwanasoka wa
kihispania David Aganz.
Mwanamuziki
maarufu kwa sasa aliwahi kudate na Mhispania Gerard Pique, na ndio maana yupo
katika listi hii. Mcolombia huyo anajulikana sana kwa kujua kucheza.
Naamini alikuwa akimchezea Pique Pique kila usiku kabla hawajalala.
Model
wa kibrazil Raica Oliveira ni binti mwingine aliyeingia katika mikono
ya Ronaldo na kutumalizia kipaji cha El Phenomena wetu wa soka.
Add caption |
Demu
wa zamani wa mchezaji wa Arsenal Freddie Ljunberg pia ni demu wa sasa
wa mchezaji wa zamani wa Manchester United anayeichezea Sunderland
Kieran Richardson. Ana miaka 20
Zamani
alikuwa anajulikana kama Posh Spice aka Victoria Beckham, Mke wa David
Beckham. Yeye na mumewe wanatajwa kama moja ya couples bora kabisa
miongoni macelebs walio katika mahusiano. Ndoa yao ina watoto wanne
mpaka sasa.
Popote
utakapokutana na huyu mwanamke kama wewe ni mwanaume kamili ni lazima
umtazame mara mbili. Anaitwa Yolanthe Cabau, mke wa kiungo wa Inter
Milan Wesley Sneijder.
Mrembo wa kiswidishi ameolewa na mmoja wanaosoka bora bora waliowahi kutokea katika historia ya soka, Luis Figo.
Usimuone
Diego Forlan anapiga sana mashuti ya mbali ukajua yanakuja hivi hivi
tu. Analelewa vizuri na mpenzi wake modo wa Kiargentina Zaira Nara.
Huyu
Miss England 2004 na Miss Great Britain 2006, amekuwa na mahusiano ya
kimapenzi na wanasoka kama vile Teddy Sherigham, Marcus Bent na Jermain
Defoe. Aliporwa taji lake la Miss Great Britain mara baada ya picha zake
za uchi za jarida la Playboy kutoka, pia aligundulika alikuwa na
mahusaino na moja ya majaji wa Miss Great Britain Teddy Sheringham.
Demu
wa high school wa Kaka, Carolina Celico ni mzuri hatari. Japokuwa ni
vigumu kwa wanasoka au watu maarufu kudumu na mwanamke mmoja kwa muda
mrefu lakini mlokole Kaka na utajiri pamoja na umaarufu wote alionao
hapa ndio kafika. Wameshaona na wana mtoto mmoja.
Mke
wa mwanasoka Joe Cole na vingi vya kui-offer camera. Uzuri wake ni
hatari na ndio maana haishangazi kuona Cole akiwa kaamua kumueka ndani.
Anajulikana mno kwa mahusiano yake yaliyotingisha mno ndoa ya John Terry - pia Vanessa Perroncel ndiye aliyeleta ugomvi kati ya Wayne Bridge . Ni vigumu kumlaumu Terry kwa uzuri alionao huyu binti.
English
model na mwandishi wa makala za urembo katika gazeti la Daily Mirror
ndiye mwanamke aliyeuteka moyo wa The Fantastic Captain Steven Gerrard.
Mrembo
huyu aliyezaliwa Spain ni moja kati ya wanawake wengi wanaomjua
Cristiano Ronaldo akitoka kuamka anakuwa na sura gani. Nererida Gallardo
pia amewahi kutekwa na Sergio Ramos.
Huyu
ni mrembo ambaye alishawahi kushinda tuzo ya mwanamke mzuri kuliko wote
nchini Nigeria, ameolewa na mchezaji wa Fenerbahce Joseph Yobo pia ni
mtoto wa kufikia mchezaji John Fashanu.
Anajulikana
kwa mahusiano yake yaliyowagonganisha wachezaji wa England Peter Crouch
na Shaun Wright Philips. Lauren Pope ni mjasiliamari anayefanya kazi
kama DJ katika moja ya kumbi huko jijini London.
Huyu ni mke wa kiungo wa timu ya taifa ya Argentina Martin Demichelis - anaitwa Evangelina Anderson.
Model huyu wa kibrazil anaipenda timu yake ya taifa.
Warner
alikuwa na mahusiano na Ronaldo de lima mpaka 1999. Baadae akaolewa na
golikipa wa taifa hilo Julio Ceaser na sasa wana watoto wawili.
Pamoja
na umalaya wake lakini huyu ndio mwanamke aliyeweza kumtuliza Kapteni
John Terry. Tayari ndoa imeshajibu na ipo imara japokuwa imekuwa
ikiandamwa naskendo za umalaya wa mumewe
Carlos
Tevez anajulikana kwa kujua kulisakata soka, lakini muargentina huyo
pia ni hatari kwa warembo wakali. Natalia Fassi ni mrembo mwingine
aliyeiletea kashikashi ndoa ya Carlos.
Mrembo huyo Mariana Paesani alishea chumba kimoja na Carlos Tevez kipindi mke wa carlos akiwa anamlea mtoto wao mchanga.