Home » , » MASHOGA,WASAGAJI WAFANYA SEMINA MOROGORO.TAZAMA JINSI ILIVYOKUA

MASHOGA,WASAGAJI WAFANYA SEMINA MOROGORO.TAZAMA JINSI ILIVYOKUA


, MOROGORO

WAKAZI wa mjini hapa walifurika katika Ukumbi wa Hedema pande za Msamvu, kushuhudia semina ya mashoga na wasagaji, Risasi Mchanganyiko limefuatilia kwa karibu Semina hiyo ya siku tano iliyoshirikisha mashoga 20 na wasagaji 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ilianza Oktoba 28 hadi Novemba Mosi mwaka huu.
Mwandishi wetu alitinga kwenye Ukumbi wa Hedema na kushuhudia mashoga na wasagaji hao wakipata  kifungua kinywa .
Mmoja wa mashaga hao aitwaye Ibra kutoka Lindi alidai kwamba semina hiyo imewajengea uwezo wa ufanishi wa kazi yao hiyo ya ushoga.
“ Mimi sasa nitakuwa nikitembea na kondomu zangu kwenye begi, nikipata bwana sina shida ya kumuuliza kondomu, hayo ni miongoni mwa mambo tunayoyajadili kwenye semina hii,” alisema Ibra.
Mwandishi wetu alijaribu kuingia kwenye semina hiyo lakini alizuiwa na kutakiwa kuondoka eneo hilo.
“ Humu tunajadili mambo yetu binafsi hivyo hatutaki yaandikwe ukitaka picha njoo Jumapili asubuhi tunamaliza semina yetu tutapiga picha,” alisema kiongozi mmoja wa mashoga hao aliyegoma kutaja jina lake.
Jumapili mwandishi wetu alifika kwenye ukumbi huo na kuambiwa kuwa semina hiyo iliishia Ijumaa na mashoga hao waliondoka Jumamosi.
Jitihada za kumuona  Meneja wa ukumbi huo, Bw Joseph Lukuba zilifanikiwa na alikuwa na haya ya kusema:
“ Awali sikujua kama Semina ile itawashirikisha mashoga na wasagaji kwani waliokuja kukodi ukumbi ni watu wanaojihusisha na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi ambao mara kwa mara huja kukodi ukumbi  wetu.
“Cha ajabu wakati semina ilipoanza nikashangaa kuwaona mashoga na wasagaji wamejaa ukumbini,” alisema meneja huyo.
Alipoulizwa kama anajua ajenda ya semina hiyo Lukuba alisema hajui chochote.
“Jamaa walikuwa makini hawakutaka watu kuingia hovyo kwenye semina yao lakini nahisi walikuwa wakiwapa mafunzo dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi,” alisema.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved