Mtu Huyu Ana Uzito Wa Kilo 610, Kutokana Na Afya Yake Kuhitaji Msaada
Kitaalam, kutokana na kuzidi kunona kadri siku zinavyozidi kwenda.
Mfalme wa Saudi
Arabia, ameingilia kati mpango wa kumsaidia Raia wa nchi hiyo, Khalid
bin Mohsen Shaari ambaye ndiye binadamu mnene na mzito zaidi duniani
akiwa na uzito wa kilogram 610, katika mchakato wa kumtibu na kumrudisha
katika hali nzuri zaidi.
Kutokana na unene,
ukubwa na uzito wake, Khalid hawezi kutembea wala kusogea mwenyewe bila
msaada wa kifaa maalum cha kumbeba akiwa katika kitanda chake, na cha
ajabu zaidi, Ni mshkaji mdogo tu ambaye umri wake ni kati ya miaka 18 na
20.
Kwa mujibu wa rekodi
za Guiness, Manuel Uribe kutoka Mexico ndiye aliyekuwa akishikilia
rekodi ya mtu mzito na mnene zaidi duniani ambapo alikuwa na uzito wa
kilo560, Na baada ya kuonekana na kuingizwa katika matibabu, kwa sasa
amepungua na kufikia uzito wa kilo 444.
Mfalme Abdullah tayari ametoa amri kuwa Khalid kuhamishwa huko Riyadh kwaajili ya mchakato wa matibabu yake.
TOA MAONI YAKO HAPA