Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anadhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa kichwani na kusababisha kuzirai.
Tukio hilo
limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini
mjini Singida. Awila ambaye amelazwa wodi 2 hospitali ya mkoa amedai
baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa Fedha na baada ya
kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga
na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani .
Hata
hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi.(Picha
na Nathaniel Limu).