Hii ndio coaster iliyopata ajali ambayo baada ya ajali ilihama barabarani na kuelekea vichakani.
Huu
ni upande wa mbele wa garri aina ya Suzuki Escudo ambao unaonekana
kuumia sana, na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakishangaa jinsi
ambavyo gari hiyo imeharibika.
Huu ndio upande wa mbele wa coaster iliyopata ajali na abiria wote kutoka wakiwa wazima wa afya.
ARUSHA jana
usiku majira ya saa moja ilitokea ajali mbaya iliyohusisha gari aina
ya Escudo yenye nambari za usajili T600 AUC na Coaster yenye nambari za
usajili T598 BNS. Ajali hiyo iliyotokea eneo la Makumira, wilayani
Arumeru, jijini Arusha. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema
chanzo cha ajali hiyo wamesema kuwa ni gari aina ya coaster iliyokua
ikitokea jijini Arusha na ilipofika eneo la makumira ilitaka kupita gari
iliyokuwa mbele lakini kabla gari hiyo haijamaliza kuipita gari hiyo,
kumbe mbele kulikua kuna gari aina ya Escudo iliyokua ikitokea Moshi
kuelekea Arusha ndipo zilipokutana uso kwa uso na kusababisha ajali
mbaya.
Katika
ajali hiyo hakuna hata mtu mmoja aliyefariki ila dereva wa gari aina ya
Escudo aliyefahamika kwa jina moja la Hussein maarufu kama Baunsa ndie
aliyeumia sehemu za miguuni na kichwani lakini wasamaria wema waliweza
kumtoa katika eneo la ajali na kumuwahisha hospitali