Home » » OZIL ATUA ARSENAL KWA REKODI MPYA. YA FEDHA

OZIL ATUA ARSENAL KWA REKODI MPYA. YA FEDHA


 

Arsenal wamevunja rekodi zao za kifedha jana jumatatu baada ya klabu hiyo kukubali kulipa kiasi cha  £42.5million kumsajili kiungo  Mesut Ozil kutoka Real Madrid.
Katika siku ya kukumbukwa pale Emirates Stadium, Gunners wamechangia uvunjwaji wa rekodi ya usajili kwa matumizi kuzidi kiasi cha £500million katika dirisha la usajili kwa kumleta kiungo huyo wa kijerumani kutoa Real Madrid. Ada ya uhamisho wa Ozil imevunja rekodi ya £17.5m ambayo Arsenal ililipa kwa ajili ya Jose Antonio Reyes mwezi January 2004.

Arsenal pia imemfanya kiungo huyo mwenye miaka 24 awe mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo kwa mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya £140,000kwa wiki.

Ozil alisema: ‘Naangalia mbele na maisha yangu ndani ya Arsenal Katika kuongea na Arsene Wenger, niligundua kwa haraka sana kitu ambacho nilikuwa nakikosa, kocha ameniamini kwa moyo wote. Nitailipa klabu na mashabiki katika kila mchezo. Sasa nataka kuilipa klabu kwa kushinda kombe.’

Usajili wa Ozil unaaminisha klabu hiyo imetimiza ahadi yake ya kusajili mchezaji wa daraja la juu baada ya kushindwa kwasajili h Luis Suarez, Wayne Rooney, Karim Benzema na Gonzalo Higuain.

Akimzungumzia Ozil, Wenger alisema: ‘Ni mchezaji mzuri, ambaye ameshathibitisha ubora wake katika ngazi ya klabu na kimataifa. Tumemuangalia na kumtamani kwa muda mrefu - ana kila kitu ambacho nataka mchezaji wa Arsenal awe nacho.'

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved