Showing posts with label ZANZIBAR. Show all posts
Showing posts with label ZANZIBAR. Show all posts

KAULI YA RAISI WA NZANZIBAB KUHUSU HOFU YA WANANCHI NA WAGENI HII HAPA





Znz hali shwari oct 16 2013 
Ripoti ambayo imetolewa na Farouq Karim wa ITV October 16 2013 kuhusu hali ya usalama Zanzibar, inasema Rais wa Zanzibar Dr. Ally Mohamed Shein amewahakikishia Wananchi na wageni kutokua na hofu kwa vile Serikali yake kupitia vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha amani inalindwa.
Dr Shein kwenye hotuba yake ya baraza la Idd Tunguu Zanzibar amesema Zanzibar iko kwenye amani kote Unguja na Pemba lakini bado wako wakorofi wachache ambao ndio wanavuruga na kuleta hofu kwa Wananchi na wageni.
Namkariri Dr. Shein akisema ‘nawahakikishia Wananchi na wageni wetu kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri ya kusimamia ulinzi na usalama wa nchi lakini vinategemea sana ushirikiano kutoka kwetu’

Upinzani ‘wawasha moto’ Zanzibar,wataka Chikawe ajiuzulu kwa taarifa za uongo...


  • Ni kauli iliyotolewa wakati wa mkutano wa hadhara uliovishirikisha vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi

Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe ametakiwa ajiuzulu kwa kutoa taarifa za uongo kwamba Zanzibar ilishirikishwa kabla ya Muswada wa Mabadiliko ya Katiba kuwasilishwa bungeni na kupitishwa na Bunge Septemba mwaka huu.
Msimamo huo ulitolewa na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar, Aboubakary Khamis Bakari wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliovishirikishwa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi uliofanyika Uwanja wa Kibandamaiti mjini Unguja jana.
Aboubakari alisema kwamba Zanzibar ilipokea taarifa ya awali ya mabadiliko kuhusu vifungu vinne vya Muswada wa Mabadiliko ya Katiba na kutakiwa Zanzibar itoe maoni na mapendekezo yake, jambo ambalo alisema lilifanyika kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hata hivyo, alisema vifungu vya mabadiliko ghafla viliongezwa kutoka vinne hadi 12 bila ya Zanzibar kupewa nafasi ya kujadili vifungu vinane ambavyo vina umuhimu mkubwa katika kupata katiba bora.
“Waziri nimesoma naye Chuo Kikuu mwaka 1972, Chikawe kwa hili amesema uongo vinginevyo ajiuzulu, hafai,” alisema Aboubakari.
Alisema kabla ya kufanyika Waziri akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, William Lukuvi walifika Zanzibar na kutaka wajadili vifungu hivyo kwa siku moja jambo ambalo alipinga kulitekeleza.
“Baada ya kuanza kupiga kelele, wenzetu walikuja Zanzibar wakitaka tujadili mabadiliko ya mswada,nikawaambia siwezi kujadili masilahi ya nchi kijuujuu, huko ni kuiuza nchi, siko tayari kufanya hilo,” alisema.
Aboubakari alisema marekebisho yaliyofanyika katika muswada huo na kutoa nafasi kujadili na kupitisha mabadiliko ya Katiba kwa kutumia wingi wa kura ni sawa na wazimu.
Alisema mabadiliko yoyote ya Katiba yanapaswa kutumia theluthi mbili toka pande mbili za Muungano, utaratibu ambao ndiyo umekuwa ukitumika na nchi mbalimbali zenye mfumo kama wa Tanzania. Mwananchi ilipomtafuta Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kujibu tuhuma hizo alisema Aboubakari ameudanganya umma mchana kweupe kwa vile yeye na Waziri Lukuvi walifika Zanzibar kupeleka rasimu ya muswada na si kujadili na kupokea mapendekezo papo kwa hapo.
Chikawe alisema kwamba walipokabidhi muswada pia walimtaarifu siku ya kuwasilishwa muswada huo katika kikao cha Bunge na kuwataka kutoa maoni na mapendekezo kwa wakati mwafaka kabla ya kujadiliwa na kamati ya Katiba ya Sheria ya Bunge.
Alisema kwamba nyongeza ya marekebisho ya vifungu vinane yalitokana na mapendekezo ya wabunge katika kamati na michango ya wabunge ndani ya Bunge katika utaratibu unaoruhusiwa kisheria.
“Baada ya kamati ya Bunge kukaa, Mbunge Halima Mdee wa Chadema ndiye aliyependekeza kutumika kwa utaratibu wa wingi wa kura katika kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba kama hatua ya theluthi mbili itashindwa kufikia mwafaka,” alisema Chikawe.
-mwananchi

VIDEO:SHUHUDIA JINSI PADRI ALIVYOCHAKAZWA NA TINDIKALI HUKO ZANZIBAR


Kwa mara nyingine Zanzibar imeshuhudia tukio la kumwagiwa tindikali ambapo watu wasiojulikana wamemwagia tindikali Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae,Padri Anselmo Mwan'gamba 
                                                  TAZAMA VIDEO;
                                                     


ZANZIBAR KUFUNGUA MASHTAKA DHIDI YA KAMPUNI YA GOLD STAR.


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itafungua mashtaka dhidi ya kampuni ya Gold Star, baada ya meli yake kukamatwa na tani 30 Za mihadarati aina ya bangi Kisiwa cha Malta Vessel, nchini Italia.


Hatua hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi wa Mamalaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Abdi Omar Maalim, alipozungumza ofisini kwake Mlandege Zanzibar, jana.


Maalim alisema kwa mujbu wa sheria namba 5 ya mwaka 2006 ya usafiri baharini, kampuni hiyo imekiuka masharti ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba silaha, dawa za kulevya, wakimbizi au mzigo wowote wenye biashara haramu.


Alisema wanasheria wa ZMA wataipitia sheria hiyo kabla ya kuamua kuishtaki kampuni hiyo mabaharia tisa wanaodaiwa kula njma za kusafirisha bangi, kabla ya kukamatwa huko Italia.


“Tunategemea kufungua mashtaka dhidi ya Kampuni ya Gold Star kwa kukiuka masharti ya fomu ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba mihadarati, silaha, wakimbizi au mzigo wowote haramu,” alisema Maalim.


Alisema meli hiyo ilisajiliwa Oktoba 5, 2011 na Kampuni ya Uwakala wa Kusajili Meli ya Philtex Corparation yenye kituo chake kikubwa cha biashara nchini Dubai, inamilikiwa na raia wa Marekani na Phillipines.


Maalim alisema Kampuni ya Philtex ina mkataba wa miaka 10 wa kusajili meli na SMZ, ikiwa na hisa asilimia 35 na SMZ 65.


Alisema mkataba huo ulitiwa saini mwaka 2007 na umeweka sharti kuwa, hakuna kampuni yoyote yenye mamlaka ya kusajili meli kwa niaba ya SMZ zaidi ya kampuni hiyo hadi miaka 10 itakapoisha.
 

Alisema kulingana na mkataba huo, upande wowote utakaovunja masharti kabla ya muda kumalizika utalazimika kulipa fidia ya dola 500,000 za Marekani na kusisitiza kuwa, Philtex  haina makosa kufuatia meli hiyo kukamatwa na bangi kwa vile ni uhalifu wa kawaida kama inavyotokea kwa meli nyingine.
 

Hata hivyo, Maalim alisema shehena hiyo ya bangi haieleweki hadi sasa kama ilikuwa ikisafirishwa kutoka Morocco au Uturuki na kwamba, mzigo huo haukutoka Tanzania kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
 
Kuhusu Philtex kukumbwa na misukosuko ya usajili tangu kuanza kufanya usajili kwa niaba ya SMZ, Maalim alikiri mwaka jana meli 36 za Iran zilifutiwa usajili baada ya kubainika kusajiliwa kinyume na sheria za kidiplomasia

“Iran imewekewa vikwazo na Baraza la Usalama wa UN, zilifutiwa usajili wake baada ya kujitokeza malalamiko ya Zanzibar kusajili meli za mafuta za Iran,” alisema

ZANZIBAR:YATAKA KATIBA MPYA IWARUHUSU KUJITEGEMEA KWA KILA KITU.

Kamati ya Maridhiano imetoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutaka Zanzibar ijitegemee karibu kwa kila kitu.
Maeneo inayotaka yaondolewe kwenye Muungano ni uraia na uhamiaji, sarafu na Benki Kuu, mambo ya nje na usajili wa vyama vya siasa.

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1976288/highRes/569881/-/10ih1q9/-/nasoor.jpg

Kamati hiyo inayounga mkono muundo wa muungano wa Serikali tatu inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo, iliwasilisha mapendekezo hayo juzi katika Ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema kuwa maoni hayo ndiyo mawazo ya Wazanzibari wengi.

Mapendekezo hayo yalisomwa na Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Ismail Jussa katika Kongamano la Katiba lililoandaliwa na kamati hiyo.

Msimamo wa kamati hiyo unaelezwa kuwa chanzo cha mmoja wa wajumbe wake, Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uanachama wa CCM, Agosti 26 mwaka huu.

Akisoma mapendekezo hayo, Jussa alisema kwa kuwa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar uliziunganisha nchi zilizokuwa huru, unatakiwa kuitwa Muungano wa Jamhuri za Tanzania, kusisitiza kuwa rasimu hiyo inatakiwa kueleza wazi kwamba nchi nyingine zinaweza kuingia kwenye muungano huo.

Alisema kamati hiyo imependekeza kuwa mambo ya nje yasiwe suala la muungano na badala yake nchi washirika zisimamie zenyewe eneo hilo.

Alisema kwa kuwa muungano umetokana na nchi mbili  zilizokubali kuungana na kuunda shirikisho,  msingi wa uraia wa shirikisho utokane na msingi wa mtu kuwa raia wa nchi mshirika na si kinyume chake.

“Kila nchi mshirika (Zanzibar na Tanganyika), ibakie na uraia wake na mtu kuwa na uraia wa nchi mshirika ndiko kumpe uhalali wa kuwa raia wa shirikisho,” alisema.

 Pia kamati imependekeza Rais wa muungano ambaye atakuwa na madaraka ya juu katika shirikisho lote kwa mambo yote ya Muungano, hivyo nchi washirika zinapaswa kuwa na haki sawa katika kutoa watu wa kushikilia Baraza la Mawaziri la Muungano, Bunge na Mahakama.

Alisema rasimu inatakiwa itamke wazi kwamba urais wa Muungano utashikwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya nchi washirika yaani Tanganyika na Zanzibar na kwamba Rais atangazwe mshindi baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 50 kutoka Tanganyika na Zanzibar.

Alisema badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa Makamu wa Rais kupatikana kutokana na mgombea mwenza, marais wa nchi washirika (Zanzibar na Tanganyika) moja kwa moja wawe makamu wa kwanza  na makamu wa pili wa Rais wa Muungano.

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved