Home » , , » WAASI WA M23 WASALITI AMRI NA KUDAI MAZUNGUMZO NA SERIKALI .NI BAADA YA HIKI KITENDO HAPA....

WAASI WA M23 WASALITI AMRI NA KUDAI MAZUNGUMZO NA SERIKALI .NI BAADA YA HIKI KITENDO HAPA....

Wanajeshi wa serikali katika Jmauhuri ya kidemokrasi ya Congo, wanashambulia ngome ya mwisho ya waasi wa M23 katika maeneo ya milimani ,msituni Mashariki mwa nchi.
Mamia ya wakimbizi wanatoroka vita karibu na mpaka wa Mashariki mwa Congo na kuingia nchini Uganda.


















Viongozi wa kundi hilo la M23 walitoa wito kwa wapiganaji wao kusitisha vita na kuruhusu mazungumzo ya amani na serikali.
Kiongozi wa wapiganaji hao Mashariki mwa nchi ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.
Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved