
ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imeshuhudia mume wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema ambao wamenaswa laivu wakifanya ‘mambo’ gesti.
Habari zilizopenyezwa katika timu yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya leseni yake ya biashara kwa kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu hufanya biashara ya kuuza miili yao katika eneo hilo.
Ilielezwa kuwa baa hiyo huwahifadhi machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono ikifanyika mchana kweupe na usiku kucha bila kushtukiwa.
KAZI YAANZA
Ikiwa imebeba kauli ya Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kuhusiana na kukomesha biashara ya madanguro jijini, vijana wa OFM walitinga ndani ya baa hiyo kama wateja na kukamilisha uchunguzi wao ambao uliwapa jibu moja tu – biashara ya ngono inafanyika nje nje!
TAARIFA POLISI
Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa hali hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye aliwasili kituoni hapo na kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua askari shupavu wa kufanya oparesheni hiyo.
Akiwa ndani, paparazi huyo alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye chumbani huku akitoa ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha zoezi kufanyika tu.
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.
Katika pekuapekua hiyo ndipo mume huyo wa mtu akanaswa laivu chumbani na mke wa mtu huku wote wakiomba msamaha kwa kuwa wana familia zao, hoja ambayo haikuwa na nguvu.
KILA MTU ANA NDOA YAKE
Katika kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
“Chondechonde mimi nina ndoa na familia jamani. Sijui nitaweka wapi sura kwa aibu. Naombeni tuyamalize kiutu uzima,” alisikika mwanaume huyo akijitetea kwa polisi, utetezi ambao haukumsaidia.
Katika mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
SAFARI YA POLISI
Pamoja na kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.