
Mama mwenye hasira wa mmoja wa wasichana wa Uingereza waliomwagiwa acid mjini Zanzibar ameungana na bintiye nchini humo baada ya jana kuwasili kwa ndege kwenye hospitali kwaajili ya matibabu.
Katie Gee, aliyefunikwa blanket, na rafiki yake Kirstie Trup
wakiwasili kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster nchini Uingereza
kutibiwa majeraha yao
Mama huyo, Nicky Gee alionekana kushindwa kujizuia kulia baada ya kumuona binti yake Katie na rafiki yake Kirstie Trup wakishuka kwenye ambulance akiwa amefunikwa blanket.

Wasichana hao ambao wote wana miaka 18 walipelekwa kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster kutibiwa haraka majeraha ambayo baba yake Katie ameyaita mabaya yasiyoelezeka.


Wote wameungua vibaya baada ya kumwagiwa tindikali usoni wakati walipokuwa wakiingia kwenye mgahawa mjini Zanzibar.
Hilo lilikuwa shambulizi la tatu wakati walipokuwa visiwani humo. Awali mmoja wa wasichana hao alishambuliwa na msichana wa kiislam baada ya kumsika akiimba wimbo wakati wa mwezi wa Ramadhan.
