Home »
KITAIFA
» JESHI LA POLISI LATANGAZA DAU LA MILIONI 10 KWA MTU YEYOTE ATAKAYEWATAJA WATU WALIOWAMWAGIA TINDIKALI WAZUNGU WAWILI
Zanzibar, Tanzania — Kamanda wa Polisi, Kamishna Musa Ali Musa amesema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa Shilingi milioni 10/=
kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu
waliowashambulia mabinti wawili kutoka Londona, Uingereza, Kirstie Trup
na Katie Gee.
Mabinti hao walishambuliwa kwa tindikali usoni,
kifuani na mikononi siku ya Jumatano walipokuwa njiani kuelekea kwenye
chakula cha jioni.
TOA MAONI YAKO HAPA