Pichani ni walinzi wa Amani wakiwa katika moja ya doria kwenye
mitaa ya mji wa Goma, mwanzoni mwa wiki hii kumetokea mapingano
katika eneo la vilima vya Kibati Magharibi ya Kivu ambapo kundi la
waasi la M23 lilishambulia walinzi wa amani wa Misheni ya Kutuliza
Amani katika DRC ( MONUSCO) waliokuwa katika Operesheni ya kulinda raia
wakishirikiana na Majeshi ya Serikali ya DRC. Shambulio hilo
limesababisha mwanajeshi Mtanzania kupoteza maisha na wengine 10
wakiwamo wanajeshi wa Afrika ya Kusini wamejeruhiwa. Tukio la
kushambuliwa kwa walinzi hao limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ban Ki
Moon na Baraza Kuu wametuma salamu za rambirambi kwa familia ya
marehemu na familia za wale waliojeruhiwa na kwa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika ya Kusini. Aidha Baraza Kuu
limesisitiza kwamba vitendo vinavyolenga kudhoofisha mamlaka ya MONUSCO
havitavumiliwa
Na
Mwandishi Maalum
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amelaani kuuawa kwa Mlinzi wa Amani kutoka
Tanzania ambapo wengine
kadhaa wamejeruhiwa baada ya
kushambuliwa na kundi la waasi la M23 katika katika
eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kwa
mujibu
wa taarifa iliyotolewa na msemaii wa Katibu Mkuu , inaeleza kwamba. “
Katibu Mkuu analaani kwa
nguvu zote mauaji ya mlinzi huyo na kujeruhiwa kwa walinzi wengine
10 na anatoa salamu zake za rambirambi kwa familia za walinzi hao na
kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Jamhuri ya Afrika ya kusini”.
Mashambulizi
dhidi ya walinzi hao wa Amani yametokea siku ya
jumatano katika Vilima vya Kibati
Magharibi ya Kivu ambako Misheni ya kutuliza Amani ya
Umoja wa Mataifa katika DRC ( MONUSCO)
ilikuwa ikisaidiana na majeshi ya
serikali ya DRC kuwalinda raia
katika eneo la Goma ambalo lina idadi
kubwa ya watu.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, MONUSCO
ilijibu mashambulizi hayo kwa kutumia zana mbalimbali za kivita yakiwamo
makombora, mizinga na helkopta za kivita wakati majeshi ya DRC yalitumia askari
wa ardhini, vifaru na helkopta za kivita
na kwamba operesheni
hiyo bado inaendelea.
Taarifa inaeleza zaidi kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea
kuwajibika na kuhakikisha inachukua hatua zote muhimu kwa kuzingatia Azimio namba
2094 ( 2013) la Baraza Kuu la Usalama
la Umoja wa Mataifa ambalo linasisitiza
ulinzi wa raia katika eneo hilo la Mashariki ya Kongo.
Wakati huo huo , wakati mapigano
yakiendelea, Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa, katika kikao chake
kilichofanyika siku ya Alhamisi nalo limetoa tamko la kulaani vikali tukio la kuuawa kwa mlinzi wa Amani wa
Tanzania, na kutoa salamu zako za pole
kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na familia ya marehemu pamja na
wale waliojeruhiwa.
Tamko
la Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa
limetolewa taarifa hiyo baada
ya Baraza hilo kupokea taarifa
rasmi iliyowasilishwa na Naibu
Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa
Amani, Bw. Edmond Mulet
kuhusu kinachoendelea
katika DRC.
Baraza pia limelaani kwa nvugu zote dhidi ya kujirudia rudia
kwa matukio
yanayofanywa na M23 yanayolenga MONUSCO
na rais yakuwalenga raia na MONUSCO.
Na
kwa sababu hiyo Baraza Kuu la Usalama
limetaka mamlaka ya DRC kuchunguza tukio la kuuawa kwa mlinzi huyo wa Amani na
kisha kuwafikisha mbele ya sheria watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
Aidha
Baraza Kuu limerejea tena tamko lake la
kuitaka M23 na makundi mengine yenye silaha katika DRC kuacha aina zote za
machafuko na kuweka chini silaha zao. Na kwamba, halitasita kupitisha vikwazo vya nyongeza kwa yeyeyote yule ambaye
atabainika kujihusisha na fujo na machafuko na kwamba vikwazo hivyo vitahusu
pia silaha.
Aidha
wajumbe 15 wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limeipongeza MONUSCO
kwa namna ambavyo imekuwa ikitekeleza mamlaka yake na hususani ya kuwalinda
raia na limeitaka na kuihimiza MONUSCO kuendelea na wajibu wake huo huku lilikisisitiza kwamba Baraza Kuu la
Usalama halitavumilia kitendo chochote
kinacholenga kudhoofisha mamlaka ya MONUSCO.
Vilevile
Baraza limeitaka Expanded
Joint Verification Mechanism ( EJVM) kuchunguza madai ya kuwapo kwa vitendo
vya urushwaji wa makombora kuelekea nchi ya jirani ya Rwanda
Katika hatua nyingine , Muwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu katika DRC. Bw. Martin Koble naye ameelezea
kusikitishwa kwake na tukio hilo la kuuawa kwa mlinzi wa Amani wa Tanzania.
Akielezea
masikitiko yake, Bw. Martin Koble anasema, “ mlinzi huyo wa
Amani ameyatoa muhanga maisha yake ili kuwalinda wananchi wa Goma. Ninaungana na
familia ya marehemu na walinzi wenzake
katika kombania yake katika kipindi hiki
cha majonzi na wakati mgumu”.
Katika
mwaka mmoja uliopita, kundi la waasi la M23 pamoja na makundi mengine
yenye silaha mara kwa mara yamekuwa yakipambana na Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( FARD).
Ambapo Mwezi Novemba mwaka jana kundi hilo la M23 lilichukua kwa muda
mji wa Goma.
Machi
28 mwaka huu , Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio la
kuanzishwa kwa Brigedi Maalum ( FIB)
iliyopewa mamlaka ya kuyadhibiti makundi ya waasi yenye silaha
yenyewe kama FIB na au kwa kushirikiana na Majeshi ya serikali ya DRC ( FARD).
Kupitia
azimio
hilo Baraza Kuu la Usalama lilitoa wito kwa kundi la M23 kusitisha
mara moja aina zote za machafuko ikiwa ni pamoja na kuweka chini
silaha zao.
Aidha
kwa
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa
kuimarisha mamlaka ya MONUSCO pamoja na kuundwa kwa FIB kumelenga
katika kusaidia utekelezaji wa malengo ya Mpango Mpana wa Kisiasa
wa Umoja wa Mataifa kuhusu Amani, usalama na maendeleo katika DRC na
eneo
la Maziwa Makuu.