Showing posts with label yaliyojiri. Show all posts
Showing posts with label yaliyojiri. Show all posts

MZEE MAJUTO AANIKA UTAJIRI WAKE TAZAMA MALI NA MAJUMBA YAKE


 


Kwenye interview aliyofanya na Millard Ayo mzee huyu staa wa movie za vichekesho hapa Tanzania ambae mpaka sasa ameshaigiza movie zaidi ya 600, umri wake ukiwa miaka 65… alithibitisha kwamba anapokea mshahara wa milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi sasa hivi kutoka kampuni ya Steps anayofanya nayo kazi

Daladala za biashara anazomiliki Mzee Majuto ni tatu tu na anamiliki pia Noah ambayo ndio anaitumia kutembelea.

19 

10
9
5
17

MKASA MZIMA JINSI BOSI WA NSSF ALIVYOUWAWA KIKATILI CHUMBANI KWAKE,DUU TAZAMA


 BOSI wa NSSF aliyeuawa kikatili kwa kuchinjwa eneo la Moshono jijini Arusha, Regina Mushi amezikwa rasmi kijijini kwao Karansi, Kitongoji cha Ashengai,Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Jumamosi wiki iliyopita.
Akizungumza wakati wa mazishi hayo baba mzazi wa marehemu, Damas Mushi alilaani tukio la kuuawa kikatili kwa binti yake huyo ambaye miaka michache iliyopita alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuajiriwa katika Taasisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  ambapo alifanya kazi miaka miwili hadi kifo kilipomkumba Oktoba 14, mwaka huu nyumbani alipokuwa akiishi Moshono, jijini Arusha.


Regina aliuawa kinyama chumbani kwake kwa kuchinjwa na kukatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake na hadi sasa haijafahamika sababu ya kufanyiwa unyama huo.
“Siku chache kabla ya kifo cha mwanangu aliniambia kuwa ana mpango wa kuendelea kusoma kwa kiwango cha shahada ya pili lakini bahati mbaya ameuawa kikatili ni jambo la kusikitisha sana,”alisema mzazi huyo.

Ametoa wito kwa jeshi  la polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo ili kuwabaini na kuwatia mbaroni waliofanya unyama huo.
Naye baba mdogo wa marehemu, Wakili  Cornelius Kariwa amesema mauaji hayo ni kinyume cha sheria na ni kitendo cha kishetani.

Ukatili wa namna hiyo wa kumchoma mtu visu ni wa hali ya juu kwani ulisababisha kutapakaa na kujaa damu kitandani, ni ukatili uliopitiliza ambapo hata angekuwa na kosa marehemu asingepaswa kupata adhabu ya aina hiyo na kwamba kitendo hicho ni cha kulaaniwa katika jamii,” alisema wakili huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana

VIDEO:TAHADHARI KWA WALE WANAO KUZA MAKALIO YAO KWA SINDANO,TAZAMA KILICHOMKUTA MWENZENU



                                        TAZAMA VIDEO
Speaking out: Vanity hopes her experience will deter other women from having illegal butt injections She said: 'Having the infection didn't make me stop. It was only when I was faced with jail and being away from my kids.' Vanity is no longer a dancer and hasn't had injections since May 2011. She now says she wants to dedicate her life to warning others of the dangers of having illegal injections. She has written a book, Shot Girls, which charts her own experience of having illegal injections and warns against following her example. 'I wanted to tell the truth 100 per cent so people know what it really is. You can get implants but injections made freely into your butt is not legal in any sense of the word,' she said





DUUUU.MUME AJINYONGA NI BAADA YA KUGUNDUA MKEWE ANATAFUNWA NA RAFIKI YAKE,MKASA KAMILI

Askari akipanda juu ya mti kwaajili ya kuushusha mwili wa marehemu.

MOVIE YA KITANZANIA ILIYOSHINDA AWARD MAREKANI,TAZAMA HII HAPA

Nimepata Email kutoka kwa Producer Timoth Conrad ambae ni producer/writer wa hii movie ya Mdundiko yenye vichwa kama Jengua, Tinno na Dokii akisema movie yao imeshinda tuzo kwenye Silicon Valley African Film Festival (SVAFF) huko California, Marekani.

Baada ya kuipata email, nimeingia kwenye website ya tuzo zenyewe na kukuta ni kweli na list nimeiweka hapo chini.

Kwenye hii email, Conrad kutoka Timamu Effects amesema ‘kwa sasa tunasubiri matokeo yatakayotoka nchini UK ambapo pia MDUNDIKO inashindanishwa tarehe 16 Novemba 2013 ikiwania FILAMU BORA YA ASILI.
Timoth ni miongoni mwa Watanzania wachache sana ambao walipata mafunzo ya kutengeneza filamu kutoka kwa wale raia wa Marekani ambao waliwahi kutengeneza filamu kubwa sana zilizochukua headlines Afrika kama Yellow Card na nyingine ambapo mafunzo aliyoyapata yalikua ya mwezi mmoja na wiki mbili.

Ukitaka kujua utofauti wake mkubwa na maproducer wengine Tanzania tazama hiyo trailer ya movie ya Mdundiko hapo chini, movie inatarajiwa kutoka wiki chache kutoka sasa.

Hii hapa chini ndio list ya movie nyingine zilizoshinda pamoja na nchi zinakotoka..

YAFAHAMU MADHARA YATOKANAYO NA VYOO VYA KUKALIA HAYA HAPA......


Waswahili husema, ‘nyumba ni choo’, wakiwa na maana kuwa nyumba haiwezi kuwa kamili bila kuwa na huduma hiyo ya choo.


Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa choo, lakini si kila nyumba iliyo na choo au hata zile ambazo zina huduma hiyo, basi vyoo ni vibovu, havina hadhi. Zipo aina mbalimbali za vyoo kwa matumizi ya binadamu katika maisha yake ya kawaida.


Vyoo vina matumizi mengi ingawa bado watu wengi hasa katika nchi maskini na zinazoendelea ikiwamo Tanzania wanatumia choo cha kuchuchumaa wakati wa kujisaidia, lakini mijini na katika nchi zilizoendelea, wao hutumia vyoo vya kukaa.

Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’.
Mgunduzi wa vyoo vya aina hii, Thomas Crapper anasema kwa mtazamo wake aliona kukaa wakati wa kujisaidia ni utambulisho wa ustaarabu na maendeleo.


Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa kuwa mkao huo unaweza kuleta matokeo mbalimbali ndani ya mwili.


Utafiti uliofanywa na mtandao wa ‘naturesplatform’ umegundua kuwa matumizi ya choo cha kukaa huweza kusababisha matatizo mbalimbali ikiwemo kansa ya utumbo mkubwa.


Mtaalamu wetu wa afya wa gazeti la MWANANCHI, Samwel Shita anasema, madhara ya vyoo vya kukaa ni makubwa kwani wakati mwingine yanaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa kutokana na haja kubwa kubaki kwa muda mrefu katika utumbo huo.


Shita anasema mtu anapojisaidia haja kubwa katika choo cha kuchuchumaa, kinasaidia haja yote kutoka kwa sababu ya msukumo unaosababishwa na mkao huo.


“Unapokaa unakuwa umekaa katika choo mwili unakuwa umelegea, hivyo inabidi utumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tofauti na unapochuchumaa,” anasema Shita na kuongeza:
“Matatizo huanza hapo, unapojisaidia ukiwa umekaa na kulazimisha kujikamua unaweza kusababisha vimishipa vidogo katika utumbo mpana sehemu ya haja kubwa ya ndani na ya nje kuvimba na maumivu makali husababishwa na ugonjwa unaojulikana kama ‘hemorrhoid,” anasema.


Anasema ‘hemorrhoid’ ni ugonjwa ambao pia huitwa bawasiri. Mgonjwa hupata uvimbe katika njia ya haja kubwa na hivyo kupata maumivu wakati wa kujisaidia na haja yake mara nyingine huambatana na damu.


Aidha, anasema vyoo hivi pia vinaweza kuwa chanzo cha magonjwa yanayotokana na shambukizi katika utumbo mpana, kitaalamu ‘Inflammatory Bowel Disease’.


“Kila binadamu anapaswa kujisaidia na kuhakikisha haja yote imetoka na kwisha kabisa, inapobakia inaweza kusababisha maambukizi katika utumbo mpana kwa kuwa ule ni uchafu wenye mchanganyiko wa vitu vingi,” anasema Shita.


“Haja kubwa inapokuwa tayari imeshajitengeneza inapaswa kutoka yote, kama itabaki kipindi kirefu inaweza pia kuleta uambukizi katika utumbo mkubwa na hata katika kidole tumbo,” anasema Shita.


“Uchafu huu si tu unaweza kusababisha maambukizi, lakini pia unaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa. Wote tunajua kuwa mkusanyiko wa sumu mbalimbali mwilini unakuweka katika hatari ya kupata saratani, hivyo tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi mapema linaweza kufikia huku,” anasema Shita.


Daktari Berko Sikirov kutoka Misri ambaye alifanyia utafiti matumizi ya vyoo vya kukaa anasema kuwa iwapo mtu ana tatizo la vivimbe vya ‘hemorrhoid’ linaweza kumalizika iwapo ataacha kutumia vyoo vya kukaa.


Hata hivyo, anasisitiza kuwa tatizo hili linaweza kwisha kama litakuwa katika hatua za awali. Kwa wenye tatizo lililokomaa watalazimika kufuata matibabu kulingana na ukubwa wake.


Dk Sikirov anaongeza kuwa mbali na kupata vivimbe, pia mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutokupata choo kwa muda mrefu.


Anabainisha kuwa kitendo cha haja kutoka kidogo na nyingine kubakia husababisha kuganda katika ukuta wa utumbo na zoezi hilo huendelea mpaka kuwa tatizo sugu.


“Haja kubwa huganda katika kuta za utumbo, hali hii huifanya haja izunguke kwa muda mrefu na ndiyo tatizo hili huanzia hapa,” anasema na kuongeza:
“Unapojisaidia ukiwa umekaa, ile njia ya haja kubwa huwa kama imejifunga, inabidi utumie nguvu nyingi sasa ukiwa na tatizo hili la kukosa haja kubwa huifanya itoke kwa uchache zaidi,” anasema Dk Sikirov.


Aidha, anasema kupata haja kubwa mara kwa mara ni muhimu kwa kuwa usipoitoa maana yake inazungusha sumu katika damu jambo ambalo ni hatari kwa afya.


Anaongeza kuwa kutopata haja kubwa ni kichocheo chenye uwezo mkubwa wa kusababisha saratani ya utumbo mkubwa na uambukizi katika kidole tumbo.


Tafsiri ya kitabibu inasema hali ya kukosa haja kubwa ni pale mtu anaposhindwa kuipata angalau mara tatu kwa wiki. Hata hivyo, ili ujue afya yako ni njema unapaswa kuwa unapata haja kubwa angalau mara moja kila siku.
Daktari Denis Burkitt aliwahi kuandika kitabu cha maelekezo ya chakula ili kuepuka ugonjwa wa saratani. Katika kitabu hicho alieleza namna ambavyo watu wanaweza kujikinga na saratani za aina mbalimbali.


Akizungumzia saratani ya utumbo mpana pamoja na kuelezea vyakula na aina ya maisha, pia aliwaasa watu kutumia choo cha kukaa ili kujiepusha na tatizo hilo.


Anaeleza kuwa kwa Marekani pekee, watu zaidi ya 150,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa.


Mtaalamu wa Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Kisali Pallangyo anasema matumizi ya vyoo hivyo yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa ya ngozi. Profesa Pallangyo anasema ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngono na ngozi kwa urahisi pale unapotumia vyoo vya kukaa tofauti na vile vya kuchuchumaa.


Aidha, anayataja magonjwa yanayoweza kuwambukizwa kwa kutumia vyoo vya kukaa kuwa ni kaswende, harara, mba, kisonono, upele na mengine.


“Mtu mwenye magonjwa ya ngozi au ya ngono, anaweza kuyaacha katika ‘sink’ anapolikalia, hivyo ni rahisi kwa mtu mwingine ‘kuyachukua’ mara atakapokaa wakati wa kujisaidia,” anasema Prof Pallangyo.


Anasema vyoo hivi ni hatari kwa afya hasa pale vinapotumika katika jumuiya na kuongeza kuwa ni bora kutumia vile vya kukaa ili kujikinga na magonjwa.




Source: MWANANCHI

KALI: MWALIMU AKUTWA NA BANGI SHULENI...SOMA KISA KAMILI...


MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Silidion Kaiza (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi gunia sita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17, mwaka huu, shuleni hapo katika kata na kijiji cha Muganza majira ya saa tano asubuhi.
Alisema kuwa raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge kwamba kuna mwalimu anajihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya, jambo walilohofia kuwa huenda akawaathiri wanafunzi wa shule hiyo kwani anazihifadhi shuleni.
Kalangi alifafanua kuwa baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika shuleni hapo na kumhoji mwalimu Kaiza, na alikiri kufanya biashara hiyo kisha akawapeleka katika moja ya darasa ambalo alikuwa akitunza bangi hiyo.
Kamanda alisema kuwa baada ya polisi kukamata bangi hiyo, waliifikisha kituoni na kwamba mwalimu huyo anaendelea kuhojiwa kisha atafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma hizo.
Aliwataka wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uuzaji wa dawa za kulevya ambavyo vimekuwa tishio kwa taifa.
-TANZANIA DAIMA

RIPOTI YA GAZETI LA RAIA MWEMA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNES MASOGANGE NA MELISA HUKO AFRIKA KUSINI...


WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.
 
Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.
 
Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.
 
Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
 
“Kusema kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo. 

"Kama zingekuwa ni dawa za kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya waliyokamatwa nayo, sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa dhamana wakati wowote kutoka sasa,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani ya Jeshi la Polisi. 

Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika Kusini tangu Julai, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine, Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo katika kundi la dawa za kulevya.
 
Ni sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.
 
Vyanzo vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa dhamana.
 
Kwa mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
 
Gazeti hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
 
“Unapozungumzia vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.

“Mtu anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini anaweza kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo kwenye kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali mbalimbali lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.
 
“Mtu akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu. Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza. 

Hiyo ndiyo adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya uhalifu, basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za Kichina.
 
Mwaka 1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
 
Raia Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.

Hata hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo wa molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.
 
“Haya mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye thamani ile. 

Tunawatafuta wahusika na tukipata taarifa tutawapa,” alisema Nzowa ambaye anatajwa kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii dhidi ya dawa ya kulevya.

BINTI AMCHOMA KISU BABA YAKE KWENYE PAJI LA USO,KISA NGONO...


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya ngono na masomo.


Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha hivi karibuni nyumbani kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi alisema alifanya kitendo hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.

“Binti yetu huyu amekuwa akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya aache vitendo vya umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa akiendeleza tabia yake hiyo ambayo sisi wazazi tumeona ni kudharau maagizo yetu,” alisema Fatuna.

Aliongeza kuwa, tabia hiyo ilikuwa ikimfanya mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kutorudi kabisa.

Mama huyo alisema, kutokana na tabia hiyo waliamua kumdhibiti ili aache lakini matokeo yake alimchoma kisu baba yake na akamsingizia alitaka kumbaka hali iliyowalazimisha polisi kuwaweka ndani wote.

Fatuma alikwenda mbali zaidi kwa kuwaomba baadhi ya wanajeshi ambao wana uhusiano wa kimapenzi na binti huyo waache kwa kuwa ni kinyume cha maadili na mwanaye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne.

Maelezo ya denti huyo yalimfanya baba mzazi kuahidi kujiua baada ya kutoka kituoni hapo akidai amedhalilishwa sana, hali iliyowafanya polisi kuamua kuendelea kumshikilia licha ya kwamba walishamruhusu kutoka baada ya mkewe kumtetea.

Afisa mmoja wa jeshi la polisi ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Tunaendelea na uchunguzi na wote wawili, baba na mwanaye tunawashikilia ili kubaini chanzo cha kutokea kwa tukio hilo, baada ya uchunguzi maelezo zaidi utapewa na kamanda wa mkoa afande Liberatus Sabas, kwani ndiye msemaji wa jeshi mkoani hapa,” alisema afisa huyo

MWANAMUZIKI WA TAARABU AHMED MGENI AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI...

Mwimbaji wa kundi la Zanzibar Njema Mordern Taarab Ahmed Mgeni amefariki dunia leo alfajiri (September 17) katika Hospitali ya Mnazi mmoja, Kisiwani Zanzibar alikolazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua.

Akiongea katika kipindi cha Leo Tena ya Clouds Fm mkurugenzi mwenza wa Zanzibar Njema Modern Taarab Ally Ngereja amesema msiba uko Amani Fresh, Zanzibar ambapo ni kwa baba yake na atazikwa leo (September 17) saa kumi jioni.

Marehemu aliwahi kutamba na nyimbo nyingi ikiwemo sitetereki inayofanya vizuri mpaka sasa.

MH WILLIAM LUKUVI :AZOMEWA NA WABUNGE WAKATI AKIJIBU SWALI LA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA.



WATANZANIA 247 wamekamatwa katika nchi mbalimbali duniani na wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, William Lukuvi, alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM).
Katika swali hilo, Magige aliitaka Serikali ieleze ukubwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini na ukoje na kuhoji kama haioni kuna tatizo katika ukaguzi wa abiria na mizigo kwenye viwanja vya ndege wanakopita watuhumiwa.
Mbunge huyo pia aliitaka Serikali, ieleze imefanya juhudi gani za kukabiliana na hali ya upitishwaji wa dawa hizo.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo nchini, unadhihirishwa na idadi hiyo ya watuhumiwa Watanzania wanaoshikiliwa nje ya nchi kuanzia 2008 hadi Julai 2013.
Mbali na Watanzania hao nje ya nchi, Lukuvi alisema nchini kuna wageni wapatao 31 wanaoshikiliwa mahabusu katika magereza ya Keko na Ukonga.
Baada ya kutoa ufafanuzi huo, Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse (Chadema), aliomba kuuliza swali la nyongeza ambapo aliitaka Serikali kutaja kwa majina wahusika katika biashara ya dawa za kulevya.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema kazi ya Serikali si kutaja majina, bali kuyapokea na kuyafanyia uchunguzi na mwisho kuchukua hatua za kisheria.
“Si kazi ya Serikali kutaja wahusika bungeni, lakini tunachofanya kwa ambao wanatajwa ni kuwapeleka katika vyombo husika na kuendelea na uchunguzi na wakithibitika ndipo wanatajwa na kuchukuliwa hatua.
“Tukisema tuwataje, hata humu ndani wabunge wote watakwisha maana wako kwengi wanaotajatajwa. Hata gazeti la Jamhuri limetaja maana wenzetu wanao ushahidi nao, na wale wasioridhika wanaweza kwenda kushitaki.
Hivyo walio na majina na vielelezo watuletee ili tuwashughulikie. Baadhi ya wabunge walionekana kuguna na kuzomea pale Lukuvi alipokuwa akitoa ufafanuzi wa suala hilo, jambo lililomfanya Spika Anne Makinda, kukemea hali ya zomeazomea ndani ya Bunge.
Hivi karibuni, vita dhidi ya dawa za kulevya, imekuwa gumzo baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuapa kuzuia uchochoro wa kupitisha dawa hizo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kwa kuanzia, Dk Mwakyembe alitaja maofisa alioagiza wafukuzwe kazi na kufunguliwa mashitaka ya jinai chini ya Sheria ya Kuzuia Dawa za Kulevya, kwa tuhuma za kupitisha dawa za kulevya katika uwanja huo.
Maofisa hao ni pamoja na Maofisa Usalama, Yusufu Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana. Mbali na maofisa hao, pia aliagiza Jeshi la Polisi kumwondoa mara moja katika uwanja huo, askari Polisi, Koplo Ernest na kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kushiriki kwake kwenye njama za kupitisha mabegi sita ya dawa za kulevya, yaliyokamatwa Afrika Kusini.
Pia alisema Polisi inapaswa kumsaka Nassoro Mangunga, aliyekwepa vyombo vya Dola vya Afrika Kusini na kutoroka na mabegi matatu ya dawa hizo. Dk Mwakyembe alisema mbeba mizigo katika uwanja huo, Zahoro Seleman, anapaswa kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashitaka, ili aunganishwe na wenzake kujibu mashitaka ya jinai.
Dk Mwakyembe pia aliiagiza Idara ya Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina kwa maofisa wake waliokuwa zamu siku ya tukio, kwa kuchelewa kufikisha mbwa wakati mwafaka kukagua mabegi hayo na kuliletea Taifa fedheha kubwa

PROFESA MMOJA WA CHUO CHA UDSM MBARONI KWA KUJERUHI KWA RISASI....!!!




Professa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ramadhani Senzota, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumjeruhi kwa risasi fundi ujenzi, aliyefahamika kwa jina la Fadhili Mkachini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10:50 jioni eneo la Tegeta Salasala, wakati Fadhili na mafundi wenzake wakiendelea na ujenzi.

Kamanda Kova alisema tukio hilo lilitokea baada ya mafundi hao wakiendelea na ujenzi wa nyumba ya mtu anayetambulika kwa jina la Khadija, ndipo Profesa huyo alitokea na kuwataka wasitishe shughuli hiyo.

Kova alisema kabla ya mafundi hao kufanya chochote, Profesa huyo alichomoa bastora aina ya Akidali Mini yenye namba 03 TZ CR 92277, iliyokuwa na risasi saba ndani ya magazine na  kumpiga fundi huyo tumboni na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo, Profesa Senzota anashikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi na fundi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akipatiwa matibabu.

Wakati huo huo, watu saba wanaosadikiwa kuwa majambazi wanashikiliwa na Polisi kwa kufanya uhalifu wa kutumia silaha, sare za polisi na redio ya mawasiliano katika maeneo ya Boko, Tegeta, Mbweni, Bahari Beach na maeneo mengine ya Jiji.

Watuhumiwa hao ni Khamis Mkalikwa (40), Magila Werema (31), Nurdin Bakari (46), Materu Marko (32), Louis Magoda (34), Amos Enock (23) na Amir Mohamed (45), wote wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Kamanda Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa jana katika eneo la Kiluvya, Wilaya ya Kinondoni na walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Cresta GX 100, yenye namba za usajili T 546 BWR.

Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walikutwa na bastora moja aina ya Brown B.3901, ambayo ilikutwa na risasi nne na ganda moja la risasi, sare za polisi pea mbili na moja yenye  cheo cha Stesheni Sajenti na nyingine ikiwa na beji inayosomeka kwa jina la SSGT A.M.Mduvike.

Kova alisema watuhumiwa wawili kati ya saba wamejeruhiwa na wapo hospitali kwa matibabu na uchunguzi dhidi yao bado unaendelea.

Katika tukio lingine, mtu aliyetambulika kwa jina la Alquine Masubo (42), anashikiliwa na polisi kwa kosa la kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwamo kitambulisho cha JWTZ namba 7001-E.1075, bastola aina ya Browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine, pia alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na bastola nyingine aina ya MAKNOV yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 na bastola moja ilikuwa na umiliki na nyingine ilikuwa haina.
 

CHANZO: NIPASHE

ALITAKA KUSHINE IDD MKE WA MTU ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUNASWA AKIIBA NGUO KARIAKOO

Jimama mwenye hadhi yake ambaye ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Mary au Mama Gilo, mkazi wa Sinza jijini Dar amekula kichapo cha kutisha almanusra apoteze uhai baada ya kunaswa akiiba nguo kwa ajili ya Sikukuu ya Eid El Fitr. 
Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilijiri katika moja ya maduka makubwa ya nguo Kariakoo, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.

TAMBUA SABABU ZA WATOTO WACHANGA KULIA, HIZI NDIZO SABABU ZAKE !!!!..

Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.

Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka ? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. 

MAAJABU,MWANASHERIA AISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU...!!

Maajabu mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee . Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo .

MANGE KIMAMBI "NIKIJA BONGO LAZIMA NIVAE HELMENT YA KUZUIA TINDIKALI" ...

"Duh Bongo pamechafuka aiseeee....................................................................................................
Nafuu yake ana pesa za kukodi private jet to SA within 1 hr ya kumwagiwa tindikali...
Maana angetibiwa bongo yawezekana ange poteza macho yake yote mawili......
Duh... Inatisha sana....

KODI YA SIMU KURUDI BUNGENI AGOSTI MWAKA HUU KWA AJILI YA KUJADILIWA UPYA

 SAKATA la kodi ya simu ya Sh 1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayolipwa na watumiaji wa simu, litamalizwa bungeni kisheria. 
Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesema wameanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala wa kodi hiyo.

MAPACHA WANASWA LIVE WAKISAGANA,LAANA TUPU...!! .

Ama kweli dunia imekaribia kwisha. Wasichana wawili kulwa na doto,toka nitoke waishi kinyumba kiasi cha kulivuruga tunda la mti wa katikati huku kulwa akijifanya mume na doto akijifanya mke.
Taarifa za kina zinasema walianza tabia hiyo mbaya katika hoteli moja ya kitalii iliyopo Bukoba mkoani Mara.

MAITI YAIBWA, KABURI LAKUTWA WAZI...!!

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, familia ya Said Abdallah inayoishi Buguruni jijini Dar es Salaam imelazimika kutokwa machozi upya baada ya maiti ya mtoto Sophia Said (1) aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria, kuibwa na watu wasiojulikana na kaburi lake kuachwa wazi, Uwazi limechimbua.


BODI YAKANUSHA UVUMI KUWA WALIOOMBA MKOPO WA ELIMU WANAPASWA KUJIANDIKISHA UPYA...!!.

Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.

Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.

Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni
mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz

Tangazo hili limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.
 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved