Showing posts with label KENYA. Show all posts
Showing posts with label KENYA. Show all posts

KENYA:MAPIA YA IBUKA USAFIRI WALIOTUMIA MAGAIDI WA WESTGATE WALETA GUMZO KUBWA.HABARI KAMILI

Standard Media wametoa taarifa nyingine ambayo inazidi kulipa shambulio la Westgate nguvu ya kuendelea kumiliki vichwa vya habari baada ya kuripoti kwamba Magaidi waliofanya hilo shambulio Nairobi mwezi September walitumia helikopta ambayo inamilikiwa na mwanasiasa maarufu wa zamani nchini Kenya ambae taarifa hii haijamtaja.

Imefahamika, sita kati ya magaidi walitumia helikopta hiyo kutoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab mpaka Nairobi kwa kuhofia kushtukiwa mapema na kukamatwa iwapo wangetumia usafiri wa ardhini.

Wapelelezi wamesema wanaamini kwenye helikopta hiyo, magaidi hawa walibeba baadhi ya silaha za kivita ambazo zilitumika kwenye shambulio hili ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya watu 60 akiwemo ndugu wa Rais Uhuru Kenyatta.

Magaidi hawa wanaaminika kuingia kwenye kambi ya Dadaab wakitokea Somalia miezi sita iliyopita ambapo walijifanya Wakimbizi huku wakiendelea kupanga shambulio la September 21 ambapo baadae walichukua hiyo helikopta ambayo tayari Pilot wake alikamatwa na kuhojiwa na kisha baadae kuachiwa.

Hata hivyo imegundulika pia ndani ya jumba la Westgate ambalo ndani yake lina maduka na migahawa mbalimbali, kwenye floor ya kwanza kulikua na raia wa Uturuki ambae alikodi chumba cha duka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuanza kukitumia kwa biashara ya kuuza simu miezi sita iliyopita na pia chumba hichohicho kutumika na magaidi kama sehemu ya kuhifadhia silaha.
Raia huyu wa Uturuki alisafiri kwenda nje ya Kenya siku moja kabla ya shambulio la Westgate na Polisi wanaendelea na msako ambao pia unalihusisha gari aina ya BMW ambalo lilimilikiwa na yeye na kutumika kubeba Magaidi hawa kwenye mizunguko mbalimbali ya Nairobi.

Kwa kumalizia post hii, kingine cha kukwambia ni kuhusu Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Wanjiru kutoka kijiji cha Kangari huko Nyeri kugundulika kwua mmoja wa Magaidi na mpaka sasa Watu wa usalama wanandelea kufatilia kama na yeye aliuwawa kwenye majibizano ya risasi kati ya magaidi na vikosi vya

HAWA NDIO MAKOMANDOO WALIO MUANGAMIZA KIONGOZI WA AL SHABAAB,TAZAMA HAPA

MAKOMANDOO sita wa Jeshi la Marekani, wakiwamo wawili walioshiriki kumuua Kiongozi wa Al Qaeda, Osama bin Laden, wamefanikiwa kumuua kinara wa kundi la Al Shabaab anayedaiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi katika jengo la biashara la Westgate mjini Nairobi nchini Kenya mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu 68 na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, aliyeko ziarani nchini Indonesia, aliwaambia waandishi wa habari jana, kuwa gaidi huyo aliuawa wakati wa mapambano kati yake na makomandoo hao. Hata hivyo, hakumtaja jina.

John Kerry alisema “Jumamosi iliyopita, makamandoo hao wa Marekani, walishambulia nyumba ya kiongozi huyo mjini Barawe, Somalia. Mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani nchini Libya na Somalia, yanaonyesha dhamira ya Serikali ya Marekani kuwasaka magaidi.”

Alisema kwamba, taarifa za kiintelijensia, zinaonyesha kinara huyo ambaye alikuwa mshirika mkuu wa Kundi la Al-Shabaab, alihusika moja kwa moja katika shambulio la kigaidi katika jumba la maduka la Westgate.

Kerry alisema kwamba, baada ya kumaliza kazi hiyo, wanajeshi hao waliondoka mjini Barawe na kurudi Marekani.


Ni katika operesheni hii ambapo pia makomandoo wa Marekani walimkamata kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda, Anas al Libi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Anas al-Liby, anahusishwa na matukio mengi makubwa yakiwamo ya kuwavizia watu wenye asili ya Marekani kuwakamata na kuwafanyia vitendo vya kinyama

KENYA YAPATA HISIA TOFAUTI KUTOKANA NA KAULI YA MAREKANI AMBAYO INASEMA........



Baada ya magaidi kuvamia kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya wiki iliyopita  ,Marekani imetoa onyo kwa raia wake kuacha kusafiri kuelekea nchini humo.

Kitendo hicho kilipokelewa kwa hisia tofauti na Serikali ya Kenya kwa kudai kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani  sio sahihi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ililaani vikali hatua ya Marekani ya kuwaonya raia wake kufanya safari nchini Kenya.

Taarifa hiyo iliitaja hatua hiyo kuwa, haina umuhimu na pia ilitolewa katika wakati ambao sio mwafaka.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa, shambulizi la Westgate jijini Nairobi, ni tatizo la ulimwengu mzima hasa kwa kuzingatia kuwa, hata Marekani yenyewe imekwishaathiriwa na vitendo kama hivyo vya kigaidi.

MAGAIDI WESTGATE WATOROKEA KUPITIA HANDAKI NDANI YA JENGO.NAMNA HII


As Kenya and foreign detectives continue to comb the Westgate debris in search of missing bodies and answers to the Westgate terror attack, shocking revelations have emerged that may catch Kenyans unaware following the 4-day horror they went through.

This is after detectives discovered a huge underground tunnel, also used as sewerage tunnel, which runs several metres from the Westgate Mall to the neighboring Nakummatt Ukay Mall.

The detectives noted that the Al-Shabaab terrorists are likely to have escaped through the tunnel, and left their explosives in the Westgate Mall, whose explosions have continued to be heard even after the Kenya Defence Forces secured the Westgate Building.

According to impeccable sources from the intelligence community, KDF did not kill any Westgate terrorist after all, because there is no sign of any of them in the debris even after combing the rubble for days now.

This comes as KDF through Interior Cabinet Secretary, Joseph Ole Lenku, insist they killed five terrorists, but have since failed to prove their assertion.


The Kenyan DAILY POST

IDADI YA WALIOFARIKI WESTAGE YALETA UTATA NAMNA HII


Watu wakiangalia majina ya waathirika katika Hospitali ya MP Shah, Nairobi. Picha ya AFP
Nairobi. Hatua ya Kundi la Al-Shabaab la Somalia kudai kwamba watu 137 lililokuwa limewateka waliuawa kwa silaha za sumu juzi, imezidisha utata wa idadi ya vifo vilivyotokea baada ya shambulizi la kigaidi lililofanyika Westgate, Nairobi, Jumamosi iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na kundi hilo kupitia kwenye mtandao wa Twitter jana, ilidai kuwa mateka 137 waliokuwa wanashikiliwa na wafuasi wao kwenye jengo la biashara la ghorofa nne, walifariki baada ya kupuliziwa sumu na vikosi vya usalama vya Serikali ya Kenya.
Hata hivyo, Msemaji wa Serikali ya Kenya, Manoah Esipisu alikanusha vikali madai ya kundi hilo.
Ghorofa tatu kati ya nne za jengo hilo zilianguka jana lakini kumekuwa na utata wa idadi ya waliokuwamo ndani.
Esipisu alisisitiza kuwa kuta za jengo hilo zilianguka baada ya magaidi hao wa Al-Shabaab kuchoma moto bidhaa za maduka hayo. “Hawa jamaa walikusanya vitu vingi kwenye ghorofa ya tatu na kuvichoma moto. Wingi wa vitu ulisababisha kuta na sakafu za ghorofa zile kuzidiwa uzito.
“Kuta za ghorofa ya tatu zikaangukia ghorofa ya pili. Kuta za ghorofa ya pili zikaangukia ile ya tatu ndiyo sababu kuu ya hali hiyo... Al-Shabaab wanajulikana kwa propaganda zao, hakuna ukweli wowote kuhusu habari hizo,” alisema Esipisu.
Kundi hilo la Al-Shabaab lilidai kupitia mtandao wa Twitter kuwa Serikali ilipuliza sumu kabla ya kuanza kubomoa jengo hilo.
Utata wa idadi ya waliokufa
Wakati Kundi la Al-Shabaab likidai kuwa watu 137 wamekufa jana, Serikali ya Kenya imeeleza kuwa watu waliokufa ni 67 tangu shambulizi hilo lilipotokea Jumamosi iliyopita.
Idadi kubwa ya waliofariki ni raia wa Kenya na wageni 18 kutoka Ufaransa, Canada, Uholanzi, Australia, Peru, India, Ghana, Afrika Kusini na China. Raia watano wa Marekani nao wamethibitika kufariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, watu 175 walijeruhiwa katika shambulizi hilo huku watu 60 wakiwa wamelazwa hospitalini.
Pamoja na watu hao, pia kuna magaidi watano waliouawa wakati wa operesheni hiyo.
Askari wanaendelea na operesheni ya kupekua eneo hilo ili kuona kama kuna uwezekano wa magaidi wengine kujificha.
Marekani, Israel na Uingereza zaongeza nguvu
Marekani, Uingereza na Israel zimeongeza mashushushu ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.
Hiyo ni baada ya nchi hizo kuongeza maofisa wake wa usalama ambao walishirikiana na vikosi vya usalama vya Kenya tangu, Jumapili iliyopita.
Kazi ya kuondoa miili
Esipisu alisema pia kuwa vikosi vya usalama vinajiandaa kuanza kazi ya kuondoa miili ya watu waliofariki dunia kwenye jumba hilo.
“Kazi hii itaanza pale vikosi vyetu vitakapojiridhisha kuwa kuna hali ya usalama,” alisema Esipisu.
Kuna wasiwasi kuwa bado kuna magadi waliojificha kwenye jumba hilo lililokuwa na maduka ya kampuni mbalimbali, migahawa kadhaa, benki na jumba la michezo ya casino.
Mwananchi

VIDEO:RAISI WA KENYA AKIHUTUBIA TAIFA LAKE JUU YA UVAMIZI WA UGAIDI NCHINI HUMO TAZAMA









Kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea Jumamosi iliyopita jijini Nairobi nchini Kenya, Rais Uhuru Kenyatta ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo. Video hapo juu ni hotuba yake kwa Wakenya.

PICHA ZA MTANGAZAJI WA KITUO CHA REDIO KENYA RUHILA ADATIA MUDA MFUPI KABLA YA KIFO CHAKE WESTGATE MALL



Mtangazaji mahiri wa vipindi vya redio nchini Kenya ambaye alikuwa akitangaza kituo cha redio cha Kiss 100 nchini Kenya, Ruhila Adatia Sood, alikuwa miongoni mwa wahanga walioshambuliwa na wanamgambo wa kikosi cha Al Shabab katika eneo la westgate Mall nchini Kenya.

Kwa muujibu wa taarifa zinaeleza kwamba Ruhila alikuwa ni mjamzito wa miezi sita alipatwa na majereha kadhaa mwilini mwake baada ya kushambuliwa na Al Shabab na kukimbizwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo nchini Kenya kwa ajili ya matibabu na hatimaye kufariki dunia.

Hizi ni baadhi ya vituo vya utangazaji alivyowahi kufanya navyo kazi East Fm, Kiss 100, Kiss TV na XFM.


Hii ndio Picha ya mwisho aliyopiga mtangazaji Ruhila Adatia muda mchache kabla ya kutokea kwa kifo chake alipokuwa akitangaza kipindi cha children’s cooking katika ghorofa ya juu zilizopo studio za East Fm ndani ya Westgate Mall na baada ya hapo alipost zaidi ya picha 8 kupitia mtandao wa Instagram na baadhi ya Tweets mpaka pale taarifa zilivyosambaa kwamba mtangazaji huyo nae ameshambuliwa na Al shabab.



Unaambiwa hizi ni baadhi ya picha za mwisho alizopost Ruhila kupitia mtandao wa Instagram muda mfupi kabla ya kutokea kwa kifo chake.










Chini ni baadhi ya Tweets za watu maarufu na mashuhuri wa Kenya na sehemu mbalimbali wakitoa salamu za pole kwa familia ya mtangazaji huyo.

KENYA:BADO MECHI KALI INAENDELEA KATI YA JESHI NA WAASI NDANI YA MALL.tazama hapa



NAIROBI

Kenyan special forces are still battling "one or two" Islamist militants holed up inside Nairobi's Westgate shopping mall, security sources involved in the operation told an AFP correspondent at the scene Tuesday.

The sources said the militants were located and isolated in or around a casino located on one of the upper floors of the complex.

Sporadic gunfire and the sound of blasts could be heard coming from inside the mall at dawn, witnesses said.

The fresh fighting came some hours after the Kenyan government had declared it was in "full control" of the sprawling mall and as the siege went into its fourth day.

The security sources confirmed that a number hostages had been rescued and evacuated to a military hospital.

Somalia's Al Qaeda-linked Al-Shabaab insurgents have claimed the attack, which began midday on Saturday when the armed militants marched into the complex, tossed grenades and fired automatic weapons and sent panicked shoppers fleeing.

At least 62 shoppers and staff were killed and close to 200 wounded.

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved