Home » » Makada wa Chadema wapewa dhamana Igunga

Makada wa Chadema wapewa dhamana Igunga

Makada wa Chadema wanaokabiliwa na shitaka la kumwagia tindikali kada wa CCM,katika Jimbo la Igunga wamepatiwa dhamana.
Makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaokabiliwa na shitaka la kumwagia tindikali kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Igunga wamepatiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wilayani humo.
 

Washitakiwa waliopewa dhamana ambao wanawakilishwa na Wakili Peter Kibatala ni Avodius Justine, mkazi wa  Bukoba, Oscar Kaijage, mkazi wa Shinyanga, Rajabu Danieli, mkazi wa Dodoma, Seif Magesa, mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza na Henry Kileo, mkazi wa Dar es Salaam.

Makada hao walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo jana na kusomewa shitaka lao la kufanya kitendo hicho kilichokuwa na lengo la kusababisha madhara mwilini.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Cosmas Mboya, inadaiwa kuwa Septemba 9, mwaka juzi, majira ya usiku katika pori la msitu wa Hanihani, mjini Igunga washtakiwa hao walimwagia tindikali kada wa CCM,  Mussa Tesha sehemu za uso, puani, mdomoni na kwenye bega la kulia kwa nia ya kumsababishia madhara makubwa mwilini.
CHANZO: NIPASHE

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved