Ndugu wa Marehemu ERasto Msuya waliofika Mahakamani wakimuondoa Mdogo wa
Marehemu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kumuwaisha Hospitali
baada ya Kupoteza Fahamu muda mfupi tu baada ya Mahaka ya Hakimu Mkazi
Moshi, kuahirisha Kesi hiyo hadi Desemba 11.
Ndugu wa Marehemu Erasto Msuya waliofika Mahakamani wakimuondoa Mdogo wa
Marehemu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kumuwaisha Hospitali
baada ya Kupoteza Fahamu muda mfupi tu baada ya Mahaka ya Hakimu Mkazi
Moshi, kuahirisha Kesi hiyo hadi Desemba 11.
Mshitakiwa namba mbili, Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38),
anayetuhumiwa na wengine saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa
kumpiga risasi akitoka kwa taabu nje ya mahakama ya Hakimu mkazi Moshi,
baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu
Ndugu wa Marehemu Erasto Msuya waliofika Mahakamani wakimuondoa Mdogo wa
Marehemu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kumuwaisha Hospitali
baada ya Kupoteza Fahamu muda mfupi tu baada ya Mahaka ya Hakimu Mkazi
Moshi, kuahirisha Kesi hiyo hadi Desemba 11, mwaka huu
Washtakiwa namba 8, Ally Mussa "Majeshi" (aliyevaa suruali ya bluu) na
mwenzake wakifunika nyuso zao kukwepa Kamera ya Mpiga picha wetu, wakati
wakiondolewa Mahakamani, muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu mkazi
Moshi, kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 11, mwaka huu.
Mmoja wa Washtakiwa katika kesi ya Mauaji, anayetuhumiwa kushirikiana
na wenzake saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi
akisindikizwa na Maaskari kutoka katika mahakama ya Hakimu mkazi Moshi,
muda mfupi baada ya kesi hiyo jana kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka
huu.
Mshitakiwa, Sharif Mohamed Athuman (31), ambaye ni mshitakiwa namba moja
katika kesi ya Mauaji ya Bilionea wa Madini ya Tanzanite, Erasto Msuya
mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, akitoka
nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, muda mfupi baada ya kesi hiyo
kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Mmoja wa Washtakiwa katika kesi ya Mauaji, anayetuhumiwa kushirikiana
na wenzake saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi
akisindikizwa na Maaskari kutoka katika mahakama ya Hakimu mkazi Moshi,
muda mfupi baada ya kesi hiyo jana kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka
huu.
Washitakiwa Joseph Damian "Chusa" na mwenzake Shaibu Jumanne Saidi
"Mredi", wakimsaidia Mshitakiwa mwenzao kupanda katika Gari la Polisi
muda mfupi baada ya kesi inayowakabili ya mauaji ya Bilionea wa Madini
ya Tanzanite, Erasto Msuya kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu
Mwandishi Wetu, Moshi
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Moshi, Leo imeahirisha Kesi ya Mauaji ya
Bilionea wa Madini ya Tanzanite Jijini Arusha,Erasto Msuya (43), hadi
Desemba 11 mwaka huu.
Kesi hiyo iliyotajwa katika Mahakama hiyo kwa mara kwanza, Agosti 21,
mwaka huu, mbele ya Hakimu Mkazi, Munga Sabuni, inawakabili watuhumiwa 8
wanaodaiwa kuuwa kwa kukusudia kinyume cha Sheria ya Makosa ya jinai,
Kanuni ya 16, Kifungu cha 196.
Pamoja na idadi ya Watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika na Mauaji hayo ya
kikatili, yaliyotokea Agosti 7, katika maeneo ya Mjohoroni, wilaya ya
Hai, mkoani Kilimanjaro, kukamilika, Upande wa Mashtaka, ukiongozwa na
Wakili, Janet Sekule, uliwasilisha Maombi ya kutaka Kesi hiyo ipangiwe
Tarehe mpya ili kupisha Upepelezi kukamilika.
Wakili Sekule, alisema kuwa kutokana na uzito wa Kesi hiyo, Jamhuri
ingependa kupatiwa muda wa kukusanya ushahidi wa kutosha ambao
utawasaidia katika kesi hiyo, ombi ambalo halikupata pingamizi lolote
kutoka upande wa Washtakiwa.
“Mheshimiwa Hakimu, kutokana na uzito wa shauri la kuuwa kwa makusudi
kinyume na kanuni namba 16, kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya
jinai, inayowakabili washtakiwa namba 1 hadi 8, Jamhuri inaiomba Mahakam
yako tukufu, kupewa muda wa kukamilisha ushahidi,” alisema Sekule.
Baada ya kuridhika na maelezo ya Maombi ya Upande wa Jamhuri, Mahakama
ya Hakimu Mkazi Munga Sabuni, iliahirisha Kesi hiyo hadi Desemba 11,
mwaka huu itakapofikishwa mbele ya Mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa.
Katika Kesi hiyo, Mshtakiwa namba Tano, Joseph Damas Mwakipesile “Chusa”
(36), ambaye ni Mfanyabiashara Maarufu wa Madini anadaiwa kuwa
alishirikiana na Mshtakiwa Ally Mussa “Majeshi”, anayedaiwa kuwahi
kulitumikia Jeshi la kujenga Taifa (JKT), kabla ya kufukuzwa pamoja na
wengine 6 kumuua kwa kumpiga Risasi 13, Bilionea wa Madini, Erasto Msuya
(43).
Watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuwa mnamo, Agosti 7, mwaka huu
majira ya6:30 mchana walifanya kitendo hicho kando ya barabara kuu ya
Arusha– Moshi katika eneo la Mjohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Washtakiwa wengine ni, Sharif Mohamed Athuman (31), mchimbaji mdogo wa
madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu Jumanne Saidi maarufu
kama Mredi (38), mkazi wa Songambele, Wilaya ya Simanjiro, Jalila
Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed Jabir ‘Msudani’ au
‘Mnubi’(32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata wilayani Hai, Karim
Kihundwa (33) mkazi wa Kijiji cha Lawate Wilaya ya Siha na Mussa Juma
Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu mkoani Arusha.
Credit: Taifa Letu