Home » , , » LAANA:MZAZI MBARONI BAADA YA KUMBAKA MTOTO WAKE WA DAMU:SHUHUDIA

LAANA:MZAZI MBARONI BAADA YA KUMBAKA MTOTO WAKE WA DAMU:SHUHUDIA


MKAZI wa Kijiji cha Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara, Mohamed Ally (42) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kufikia. 

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Paulo Kimaro alidai mahakamani kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 9 mwaka huu nyumbani kwa mtuhumiwa huyo alipombaka mtoto huyo, mwanafunzi wa darasa la saba.
 
Alidai siku hiyo mke wake alitoka na aliporejea kutaka kuingia ndani alisukumwa nje na baada ya kulazimisha kuingia ndipo akagundua kuwa mumewe alikuwa anafanya mapenzi na mtoto wake huyo

Kimaro alidai kutokana na hali hiyo aliomba msaada ofisi ya kijiji cha Njoro na mtuhumiwa akakamatwa na kufikishwa polisi na baadaye mahakamani.

Mtuhumiwa alikana mashitaka na alirejeshwa rumande hadi Septemba 23 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Mke wa mtuhumiwa, Salima Hamisi aliiambia mpekuzi blog kuwa mwanafunzi huyo ni mtoto wa kulea na walimchukua akiwa na umri wa miaka miaka minne.

Kwa mujibu wa taarifa mwanafunzi huyo alifanya mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa siku ya pili jana.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved