.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha
Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin
asikiliza maoni wakati akiendesha mjadala wa namna ya ku-brand mradi wa
Demokrasi na Amani (DEP) kuelekea uchaguzi 2015 kwa Mameneja na
Wakurugenzi wa redio za jamii 25 nchini zilizohudhuria siku ya kufunga
warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na
UNDP.
Meneja wa mradi wa Amani na Demokrasi
(DEP ) kutoka UNESCO Courtney Ivins akizungumza na Mameneja na
Wakurugenzi wa redio za jamii kupata tathmini ya warsha hiyo
iliyomalizika mwishoni mwa Juma wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Washiriki wakijadiliana katika
makundi mambo mbalimbali ya kuboresha kwenye redio jamii zao katika
utekelezaji wa mradi wa DEP kuelekea uchaguzi 2015 wakati wa
kuhitimisha warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa Juma.
Mkufunzi na Mshauri wa redio za
jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa Afisa
Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi
ya UNESCO Yusuph Al-Amin wakati wa kuhitimisha warsha ya wiki moja wa
redio za jamii katika kuziandaa kuendesha mijadala ya Amani na
Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Msafiri Andrew kutoka Mpanda FM
akiwasilisha maoni ya kikundi chake nini kifanyike katika utekelezaji wa
mradi wa Demokrasia na Amani kwa redio za jamii kuelekea uchaguzi 2015.
Meneja wa Triple A FM Borry Mbaraka
akichangia maoni wakati wa kufunga warsha ya wiki moja kwa Wakurugenzi
na Mameneja wa Redio za jamii nchini iliyomalizika mwishoni mwa wiki
wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Meneja Mawasiliano wa Pangani FM
Abdullah Mfuruki akichukua matukio mbalimbali ya kumbukumbu wakati wa
kuhitimisha warsha warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO na
kufadhiliwa na UNDP iliyowakutanisha Mameneja na Wakurugenzi wa radio za
jamii 25 nchini kwa ajili ya kuwaandaa kuendesha mijadala ya Amani na
Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Sehemu ya washiriki ambao ni
Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha
hiyo ya wiki moja iliyomalizika mwishoni mwa Juma kwenye kituo cha
Habari na Mawasiliano cha Telecentre wilayani Sengerema mkoani Mwanza
iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.
Meneja wa Kituo cha Habari na
Mawasiliano cha Telecentre SengeremaFM mkoani Mwanza Bw. Felician
Ncheye akitamka kufunga rasmi warsha ya wiki moja kwa redio za jamii
katika kutekeleza mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.
Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO
Mama Rose Haji Mwalimu akigana na Meneja wa Mradi wa DEP kutoka UNESCO
Courtney Ivins mara baada ya kuhitimisha warsha ya wiki moja iliyokuwa
ikifanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema
Telecentre mkoani Mwanza mwishoni Juma.
Mameneja na Wakurugenzi wa redio za
jamii nchini kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji mara baada ya
kumalizika kwa warsha ya wiki moja kwa ajili ya kuwaanda redio za jamii
kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasi kuelekea uchaguzi 2015
iliyoandaliwa na shirika la UNESCO na kufadhiliwa na UNDP.