Mmiliki
wa ndama huyo, Neil Davy,ambaye amemshika ndama huyo aliyekufa kwenye
picha aliuambia mtandao wa NZ wa nchini humo kuwa kama yeye asingekuwepo
wakati ndama huyo akizaliwa basi ng’ombe aliyemzaa ndama huyo naye
angekufa kwani alihangaika sana wakati akizaa.
‘Ilikuwa
ni vigumu kumuangalia wakati alipokuwa anazaa,kwani hali yake ilikuwa
mbaya sana alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu aliyokuwa
akiyapata kutokana na ndama mwenyewe alivyo nilihangaika naye sana hadi
nikalowa jasho jingi,’’alisema Davy.
Davy aliongeza kuwa alidhani ng’ombe huyo angezaa mapacha lakini kutokana na sababu ambazo hajazifahamu kikazaliwa kiumbe cha ajabu kama hicho.

Davy aliongeza kuwa alidhani ng’ombe huyo angezaa mapacha lakini kutokana na sababu ambazo hajazifahamu kikazaliwa kiumbe cha ajabu kama hicho.