WATANZANIA 247 wamekamatwa katika nchi mbalimbali duniani na wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha dawa za kulevya. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, William Lukuvi, alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM).
Katika swali hilo, Magige aliitaka
Serikali ieleze ukubwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini na ukoje na
kuhoji kama haioni kuna tatizo katika ukaguzi wa abiria na mizigo
kwenye viwanja vya ndege wanakopita watuhumiwa.
Mbunge huyo pia aliitaka Serikali, ieleze imefanya juhudi gani za kukabiliana na hali ya upitishwaji wa dawa hizo.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema
ukubwa wa biashara hiyo nchini, unadhihirishwa na idadi hiyo ya
watuhumiwa Watanzania wanaoshikiliwa nje ya nchi kuanzia 2008 hadi Julai
2013.
Mbali na Watanzania hao nje ya nchi,
Lukuvi alisema nchini kuna wageni wapatao 31 wanaoshikiliwa mahabusu
katika magereza ya Keko na Ukonga.
Baada ya kutoa ufafanuzi huo, Mbunge wa
Karatu, Mchungaji Israel Natse (Chadema), aliomba kuuliza swali la
nyongeza ambapo aliitaka Serikali kutaja kwa majina wahusika katika
biashara ya dawa za kulevya.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema kazi
ya Serikali si kutaja majina, bali kuyapokea na kuyafanyia uchunguzi na
mwisho kuchukua hatua za kisheria.
“Si kazi ya Serikali kutaja wahusika
bungeni, lakini tunachofanya kwa ambao wanatajwa ni kuwapeleka katika
vyombo husika na kuendelea na uchunguzi na wakithibitika ndipo wanatajwa
na kuchukuliwa hatua.
“Tukisema tuwataje, hata humu ndani
wabunge wote watakwisha maana wako kwengi wanaotajatajwa. Hata gazeti la
Jamhuri limetaja maana wenzetu wanao ushahidi nao, na wale wasioridhika
wanaweza kwenda kushitaki.
Hivyo walio na majina na vielelezo
watuletee ili tuwashughulikie. Baadhi ya wabunge walionekana kuguna na
kuzomea pale Lukuvi alipokuwa akitoa ufafanuzi wa suala hilo, jambo
lililomfanya Spika Anne Makinda, kukemea hali ya zomeazomea ndani ya
Bunge.
Hivi karibuni, vita dhidi ya dawa za
kulevya, imekuwa gumzo baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe kuapa kuzuia uchochoro wa kupitisha dawa hizo katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kwa kuanzia, Dk Mwakyembe alitaja
maofisa alioagiza wafukuzwe kazi na kufunguliwa mashitaka ya jinai chini
ya Sheria ya Kuzuia Dawa za Kulevya, kwa tuhuma za kupitisha dawa za
kulevya katika uwanja huo.
Maofisa hao ni pamoja na Maofisa
Usalama, Yusufu Daniel Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed
Kalungwana. Mbali na maofisa hao, pia aliagiza Jeshi la Polisi
kumwondoa mara moja katika uwanja huo, askari Polisi, Koplo Ernest na
kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kushiriki kwake kwenye njama za
kupitisha mabegi sita ya dawa za kulevya, yaliyokamatwa Afrika Kusini.
Pia alisema Polisi inapaswa kumsaka
Nassoro Mangunga, aliyekwepa vyombo vya Dola vya Afrika Kusini na
kutoroka na mabegi matatu ya dawa hizo. Dk Mwakyembe alisema mbeba
mizigo katika uwanja huo, Zahoro Seleman, anapaswa kufukuzwa kazi,
kukamatwa na kufunguliwa mashitaka, ili aunganishwe na wenzake kujibu
mashitaka ya jinai.
Dk Mwakyembe pia aliiagiza Idara ya
Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina kwa maofisa wake waliokuwa
zamu siku ya tukio, kwa kuchelewa kufikisha mbwa wakati mwafaka kukagua
mabegi hayo na kuliletea Taifa fedheha kubwa