Home »
kisiasa
» CHAMA CHA CUF CHATANGAZA NAFASI ZA KAZI ...
Natoa taarifa hii ili mwanachama yeyote wa CUF
(MWANAUME AU MWANAMKE) mwaminifu, anayefahamika vizuri ndani ya chama au
katika tawi lake, mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne kwenda juu na
mwenye uwezo mkubwa wa kujitolea (Kwa sababu majukumu ya utendaji wa
chama si ajira) aombe kutumikia nafasi hii.
Katibu wa Naibu
Katibu Mkuu Bara niliyefanya naye kazi kwa miaka miwili Ndugu. Venance
Chalamila, amechaguliwa kuwa Katibu mtendaji wa taasisi ya vijana
iitwayo YALD hivyo anapumzika majukumu ya Ukatibu wa Naibu Katibu Mkuu
Bara wiki kadhaa kutoka sasa.
...
Ukiona unaweza, tuma CV yako kwenye;
cuftanzania@yahoo.com
au tuma nyaraka zilizo katika "hard
copy" kwa;
KATIBU MKUU,
THE CIVIC UNITED FRONT CUF,
S.L.P
10979,
DAR ES SALAAM.
au ziwasilishe nyaraka zako OFISI KUU
YA CUF DAR ES SALAAM iliyoko karibu na Buguruni Sokoni.
Mwisho
wa kuleta nyaraka hizi kwa njia nilizozitaja ni ijumaa 16 Agosti 2013
saa 8 Mchana.
Ninaweza kufanya kazi na mwanachama yeyote
atakayekuwa na uwezo.
Namtakia kila le heri ndugu. Venance na
namtaka aendeleze juhudi za kufanya kazi kwa bidii huko anakokwenda,
aliitumikia nafasi hii kwa weledi mkubwa na Abarikiwe sana.
J.
Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
The Civic United Front -
CUF(Tanzania Bara),
+255717536759.
TOA MAONI YAKO HAPA