Ghati
Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani
Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia
na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.
Akisimulua
mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza
vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya
Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.
“Aliniuliza
kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia,
baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha
panga lilipo kwa kidole” alisema Ghati.
Wakati
anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini
kinafuata alifiki kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda sehemu
kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama
anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.
“ Alipoipata
ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa
panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na
kunikata mguu wa kulia ukakatika kama unavyoona”alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.
Wakati
anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini majirani hawakuwahi
kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio
kama hivyo kusikika katika maeneo hayo.
“Baadaye
walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango
wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa
ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye
kuletwa hapa” alieleza .
Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
“ Nimeishi
naye kwa miaka mine sasa na tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi
vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka linguine ni baada
ya kuoa mke wa pili ambapo alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa
kunikata mguu” alisema Ghati.
Ghati
hataweza kurudiana na mume wake huyo kwa kitendo alichomfanyia kwa
vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo
jera ili ajifunze kutokana ukatili aliomfanyia.
”
Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya kutembelea kwa
kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha watoto wangu
maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula”alisema.
Wananchi
walioshuhudia kitendo hicho walionesha kusikitishwa na kukilaa kuwa
kinaendelea kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .
“ Sikifurahii
kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu
mwenzako na hii inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku
kutuona sisi ni wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa,
mahakama imuhukumu huyu mtu adhabu kubwa inayomstahili ili liwe
fundisho kwa wengine” alisema Mwita Machera aliyekuwa hostalini hapo.
Jeshi
la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio
na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na
kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.
Hata
hivyo siku mojs baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa
kusaidiana na nguvu nza wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya
Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya
Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwiata
alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.
“ Vitendo
vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa
maisha sii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa
watu japo si wote” alisema Kamugisha kwa nija ya simu.