Home » » KAHABA APEWA KICHAPO NA MALAYA WENZAKE KWA KOSA LA KUJIUZA KWA BEI YA HASARA NA MKOPO

KAHABA APEWA KICHAPO NA MALAYA WENZAKE KWA KOSA LA KUJIUZA KWA BEI YA HASARA NA MKOPO



KAHABA mmoja katika mji wa Naivasha, jimbo la Rift Valley nchini Kenya amenusurika kufa baada ya kupewa kichapo kikali  na makahaba wenzake  wakimtuhumu  kujiuza kwa bei ndogo na kuwaharibia soko.

Wenzake hao wenye hasira walimtwanga  kahaba  huyo  kwa ngumi   wakimshutumu kwa kutokuwa na ushirikiano na  kuwaharibia  soko hasa ikizingatiwa   kuwa  hivi  sasa  ni kipindi cha mwisho  wa mwezi  ambapo  mahitaji ya kununua ngono huoongezeka.


Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira kwenye kona, gizani akiwa peke yake, na kumshambulia.

“Unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza kwa bei  ya hasara.?” Mmoja wa wanawake hao alimkaripia kwa sauti ya juu.

Mbali  na  kumpa  kichapo kilichomfanya  azirai, makahaba  hao walitaka kumkeketa (kumtahiri mwanamke) kwa kutumia chupa iliyovunjika, lakini akaokolewa na walinzi wa usiku (wengi wao ni wateja wake) kabla hajafanyiwa kitendo hicho.

"Unajua huyu mama huwa ananipatia kwa mkopo siku ninazokuwa nimechacha hivyo siwezi muacha auliwe na hawa mikora” alisikika mmoja wa walinzi hao wakati wakijaribu kumuokoa mwanamke huyo.
 
Msuguano ulianza mwezi uliopita baada ya  msichana  huyo kuhamia  mitaa hiyo ,kitu ambacho kiliwakera makahaba wazoefu  wa  eneo  hilo  kwa kuwa  walimuona kama tishio kutokana na urembo wake.

Kwa mujibu wa dereva wa bodaboda anayeitwa Peter, kahaba huyo amekua ni kivutio na anayependwa na wengi kutokana na uzuri wa umbo lake na rangi nyeupe ya ngozi yake.
 
Mbali   ya  punguzo  la  bei,  inadaiwa  kuwa kahaba huyo pia hutoa  huduma kwa mkopo, kitu ambacho wenzie hawafanyi, hivyo kuzidi kuwaaribia biashara zaidi.

“Kwa kawaida, bei ni kati ya Ksh 100 mpaka Ksh 500 (kama TZ Shs 2,000 mpaka 10,000) inategemeana na mteja. Lakini “Brownie” anauza kwa hata Kshs 50 (TShs 1,000)” alidai Peter.

Idadi ya wateja wake ilikua  kwa kasi, kitu kilichopelekea wivu na chuki kutoka kwa makahaba wengine  ambao  walifikia uamuzi wa kufanya njama za kumpa kichapo  ili iwe fundisho.

Kahaba  huyo  bado yuko hospitalini  akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata  huduma zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo. 
  
 Credit: Watemi.com

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved