Victoria Mukama (10) akiwa hospitali ya rufaa mbeya baada ya kupigwa na
baba yake mzazi sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vya
ulinzi likiwemo Lungu.
Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio
hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo
akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga
wakielekea ofisini.
Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake
hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya
asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya
kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya
unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa
na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na
mkewe.
Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la
Oscar Mukama mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya
binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili
wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.
Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia
alisema tukio hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu
asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku
akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa
nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe
na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo
kwa mwanaye.
Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni
cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia
walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu
walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.
Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu
mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali
aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti
wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya
matibabu.
Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake
hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya
asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya
kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake
ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake
anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na
kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.
Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto
amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule
kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi
mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.
Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama
(10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi
Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza
kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.
Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule
iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na
fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka
kumuokoa.
Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa
huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye
namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa
na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima
sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa
ndani ya jamii.
Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha
na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri
katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa
pamoja na kuchangia mada.
Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo
kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa
kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa
anayotendewa na mkewe.
Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe
huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa
Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara
ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.