TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
1. Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na
Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu
(Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016
2. Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya
taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha
kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya
YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.
Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji
ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe
29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina
tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na
Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake
za Vodacom Premier League katika Azam Television.
3. Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada”
inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha
Klabu ya YANGA hadharani.
Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu
ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu,
havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati
ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa
vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu
zinazojionyesha wazi.
Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula
njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.
Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na
misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana
na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa
Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.
Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na
mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa
Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba
kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam
Television kurusha mechi za YANGA.
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB