MWANAMUME mmoja mwenye asili ya kenya alimuua mama mkwe wake kwa
kumpiga risasi Jumatatu usiku kabla ya kujiua kwa bunduki hiyo mjini
Barrow katika jimbo la Georgia, Amerika.
Kwa mujibu wa polisi, Jennifer Muriu, ambaye ni mkewe marehemu aliwaita
polisi kabla ya saa mbili jioni kuwapasha habari kwamba mumewe, Ian
Muriu, 33, alifyatua risasi nyumbani kwa wakwe zake.
Ndani ya nyumba hiyo, wachunguzi walipata Bi Diana Freeman, 66, ambaye
amekuwa akiishi na familia hiyo akiwa amekufa kutokana na majeraha ya
bunduki. Mwili wa Muriu wenye alama ya risasi kichwani, ulikuwa mita
chache kando ya wake Bi Freeman.
“Miili yote miwili ilikuwa kwenye zulia,” Guthas akasema.
Maafisa walisema uchunguzi umeanzishwa kubaini nia ya kitendo hicho.
“Lakini hadi wakati huu inaminika kuwa Ian Muriu aliwaua Bi Diana
Freeman na mkwewe na kabla ya kujiua kwa kutumia bunduki hiyo hiyo.
Familia ya Murui walikuwa wamiliki mkahawa wa The Spitfire katika uwanja
wa ndege mjini humo, kwa mujibu wa ujumbe kwenye mtandao wa Facebook wa
mkahawa huo. Mkahawa huo ulifunguliwa mwezi Mei 2011 na taarifa kuuhusu
imeandikwa katika toleo la mwezi huu la jarida la Georgia.
“Familia hiyo ilihamia mji wa Barrow baada ya kufanya kazi katika
mikahawa mbali mbali katika maeneo kadha duniani,” jarida hilo lasema
source gumzo la jiji