Ilidaiwa kabla
ya hapo, wakati wakicheza, kulitokea ugomvi kati yake na mwenzake aliyekuwa
akicheza naye, Nyanswi Magaigwa, baada ya Joseph kuliwa Sh 5,000.
Katika ugomvi
huo, inadaiwa Magaigwa alichukua panga na kumjeruhi mwenzake shingoni na
kisogoni, ambapo majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya na kupatiwa
matibabu kabla ya kurejeshwa nyumbani.
Kamanda
Kamugisha alisema Joseph aliendelea kupatiwa matibabu akitoka nyumbani na
ilipofika Agosti 4 saa moja asubuhi, alifariki dunia na mwili wake ulipofanyiwa
uchunguzi, ilibainika chanzo cha kifo chake ni jeraha alilopata
shingoni.
Polisi inamsaka
mtuhumiwa na raia wema wameombwa kutoa taarifa mara watakapomwona Nyanswi, ili
aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Wakati huo huo
katika kijiji cha Kinesi, kata ya Nyamunga, wilayani Rorya, mtoto Baraka Chacha
(4), amechoma nyumba wakati akichezea kiberiti.
Baraka ambaye
hakupata majeraha baada ya kuokolewa, alipokuwa akichezea kiberiti, inadaiwa
aliwasha moto godoro na kusababisha usambae katika nyumba nzima, mali ya William
Mabala.
Kamanda
Kamugisha amewatahadhalisha Wazazi kuwazuia Watoto wao kuchezea moto kwani
hasara kama hiyo imesababishwa na wazazi kutowakanya watoto wao kuchezea
moto.