Showing posts with label kidini. Show all posts
Showing posts with label kidini. Show all posts

KESI YA MCHUNGAJI GWAJIMA KUENDELEA WIKI IJAYO .kisakamili hiki........


 
 
Mahojiano baina ya Jeshi la Polisi na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima yaliyokuwa yanatarajiwa kuendelea jana, ikiwa ni siku mbili baada ya kuachiwa kwa dhamana na jeshi hilo, jana yalikwama kuendelea kutokana na kile kilichoelezwa kutoimarika kwa afya ya askofu huyo, na sasa yatafanyika Alhamisi ijayo.

Gwajima alidaiwa kuzimia wakati akihojiwa na makachero wa Polisi waliokuwa wanamhoji, alipojisalimisha alasiri ya Ijumaa iliyopita baada ya kutakiwa kufanya hivyo, kutokana na kufunguliwa jalada la malalamiko ya kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo.
 
Kutokana na hali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu usiku wakati akiendelea na mahojiano yaliyoanzia alasiri, alikimbizwa Hospitali ya TMJ, Mikocheni akiwa chini ya ulinzi wa Polisi hadi aliporuhusiwa kutoka Jumanne wiki hii na baadaye kuachiwa kwa dhamana.
 
Mwanasheria wa Askofu Gwajima, John Mallya alithibitisha kuahirishwa kwa mahojiano kati ya mteja wake na Polisi, akisema mapema jana asubuhi aliripoti Kikuo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kama alivyotakiwa kuripoti kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano.
 
Hata hivyo, alisema hakuweza kuhojiwa kutokana na kile kinachoelezwa kuwa afya ya mteja wake haijaimarika vizuri na hivyo wamepangiwa kurudi tena kituoni hapo Aprili 9 mwaka huu, yaani Alhamisi ijayo kwa ajili ya mahojiano.
 
“Mteja wangu alifika kituoni leo (jana) asubuhi kwa ajili ya mahojiano na pia kuripoti kama ilivyoagizwa siku alipopatiwa dhamana, hata hivyo afya yake bado haijaimarika na hivyo imewalazimu polisi wampatie muda zaidi hadi Aprili 9 atakaporudi tena kwa ajili ya mahojiano,” alisema Mallya.
 
Hata hivyo, Mallya alisema hali ya afya ya Gwajima imeanza kuimarika na kadri siku zinavyozidi kwenda, atakuwa na nguvu na ataendelea na kazi zake kama kawaida.
 
Mtumishi huyo alipatiwa dhamana katika Kituo cha Polisi Oysterbay na kutakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Kati kwa ajili ya mahojiano zaidi na kusubiri uchunguzi wa kesi yake ukamilike.

PAKISTANI:KANISA LALIPULIWA NA KUUA WAKRISTO 75 NA MAMIA KUJERUHIWA TAZAMA;


Wauaji wawili wa kujitoa mhanga wamelipua mabomu yao nje ya kanisa la kihistoria nchini Pakistan jana na kuua watu 75 kwenye shambulio baya zaidi kuwahi kutokea kwa Wakristo walio wachache wa nchini humo.

 Taliban wa Pakistan wamekiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea katika mji wa Peshawar, wakisema wataendelea kuwalenga wasio Waislamu hadi hapo Marekani itakapositisha mashambulizi katika mji huo wa kikabila nchini humo. 


Shambulio la hivi karibuni lilifanyika Jumapili pale makombora yalipopiga majengo mawili katika eneo la North Waziristan, na kuua watu sita wanaodhaniwa kuwa wanamgambo, maofisa wa intelijensia Pakistan walisema.
Shambulio kwenye Kanisa la All Saints, ambalo pia lilijeruhi watu 110, linatekeleza kitisho kilichotolewa na Taliban wa Pakistan wakati huku serikali ikitaka mpango wa amani na wanamgambo hao.
Shambulio hilo limetokea wakati mamia ya waumini wakiwa wanatoka nje ya kanisa hilo lililoko katika wilaya ya Kohati Gate mjini humo baada ya huduma ya kupata chakula cha bure aina ya wali.
"Kulikuwa na milipuko na kulikuwa na mateso kwetu sote," alisema Nazir John, ambaye alikuwa kanisani pamoja na takribani waumini wengine 400.
"Niliporejewa na fahamu zangu, sikuona chochote ila moshi, vumbi, damu na watu waliokuwa wakilia kwa uchungu. Niliona sehemu za miili zilizosambaratika na damu kuzunguka eneo lote."
Manusura walikumbatiana kila mmoja baada ya milipuko huko. 

Ukuta mweupe wa kanisa hilo, ambalo lilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa miaka ya 1800, ulitapakaa mashimo yaliyochimbwa na vipande vya vyuma vilivyotoka katika mabomu ma kusababisha uharibifu mkubwa.
Damu ilitapakaa sakafuni na kusambaa kwenye ukutani. Sahani zenye wali zilitawanyika kila pembe za eneo hilo.
Shambulio hilo lilifanywa na watuhumiwa wawili wa kujitoa mhanga ambao walilipua mabomu yao kwa kupokezana. Mamlaka zimekuta sehemu za mwili na zilikuwa zikijaribu kutambua umri wao.
Milipuko hiyo imeua watu 75 na kujeruhi wengine 110. Waliokufa ni pamoja na wanawake na watoto.
Idadi ya majeruhi ni kubwa mno kiasi cha hospitali hiyo kuishiwa majeneza kwa ajili ya waliokufa na vitanda kwa ajili ya majeruhi, alisema Mian Iftikhar Hussain, waziri wa zamani wa habari wa jimbo la Khyber Pakhtunkhwa ambaye alikuwa katika eneo la tukio.
"Hili ni shambulio baya zaidi dhidi ya Wakristo katika nchi yetu," alisema Irfan Jamil, askofu wa mji wa mashariki wa Lahore.
Mmoja wa waliojeruhiwa, John Tariq, ambaye amepoteza baba yake katika shambulio hilo, aliwauliza washambulizi hao, "Tumewakosea nini watu hawa? Kwanini tumekuwa tukiuawa?"
Ahmad Marwat, ambaye alijitambulisha kama msemaji wa tawi la Jundullah la Taliban wa Pakistan, alidai kuhusika na shambulio hilo.
"Wote wasio Waislamu nchini Pakistan ni walengwa wetu na wataendelea kuwa hivyo kwa wakati wote Marekani inaposhindwa kusitisha mashambulizi katika nchini yetu," alisema Marwart kwa njia ya simu kutoka sehemu isiyojulikana.
Askofu wa Peshawar, Sarfarz Hemphray, ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia shambulio hilo na kuishutumu serikali na vyombo vya ulinzi kwa kushindwa kuwalinda Wakristo wa nchini humo.
"Endapo serikali itaonesha nia, inaweza kudhibiti ugaidi huu," alisema Hemphray. "Tumekuwa tukizitaka mamlaka kuimarisha ulinzi, lakini hazitilii maanani."
Waziri Mkuu wa Pakistani ameshutumu shambulio hilo katika taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa habari, akisema, "Magaidi hawana dini na wanaolenga watu wasio na hatia ni kinyume cha mafundisho ya Kiislamu na dini zote."
"Matukio kama hayo ya kiwendawazimu ya ugaidi yanaakisi unyama na akili zisizo za kibinadamu za magaidi," alisema.

MAAJABU:ZIMBABWE MTOTO AMUOA MAMA YAKE NA KUMPACHIKA MIMBA.

Woman To Marry Her Own Son In Zimbabwe; Mother Pregnant With Son’s Child
Betty Mbereko, a 40-year-old widow who has been living under the same roof with her own son, 23-year-old Farai Mbereko is set to marry him.
The mother and son who are madly in love with each other plan to take their romance to a new level considering they’re expecting a child together.
Betty from Mwenezi in Maswingo who is now 6-month-pregnant for her son confirms that she has decided to marry him because she does not want to marry her late husband’s younger brothers, whom she says are coveting her.
Betty stunned a village court last week when she said the affair with her son had begun three years earlier.
She said after spending a lot of money sending Farai to school following the death of her husband, she felt she had a right to his money and no other woman was entitled to it.
Lord have mercy.
What is going on in this world.

ULINZI WA PONDA WAIGHARIMU SERIKALI MILIONI 10




*Usafiri wa helikopta waitafuna dola mara 71 ya gharama ya gari
ULINZI wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa gerezani na anapopelekwa mahakamani, umeanza kuvitesa vyombo vya Dola. Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, zinaeleza kuwa serikali juzi ilitumia kiasi cha shilingi 10,682,031 kama gharama za usafiri wa helikopta za kumpeleka na kumrudisha kiongozi huyo mahakamani mkoani Morogoro.

MTANZANIA Jumatano kupitia vyanzo vyake vilivyoko ndani na nje ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 hadi saa moja ni dola za Marekani 3,000 hadi 3,300 ambazo ni sawa na shilingi 5,341,032.85 .

Hivyo gharama za kwenda na kurudi kwa saa jumla yake ni dola za Marekani 6,600 ambazo ni sawa na shilingi 10,682,031.


Akithibitisha hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, Antony Mwami alisema gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 ni dola 3,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni tano.

Katika uchunguzi wake gazeti hili limebaini kuwa gharama hizo zilizotumika kwa siku moja tu, zingetosha kumsafirisha Ponda kwenda Morogoro na kurudi mara 71, endapo ungetumika usafiri wa gari wa kawaida.

Gazeti hili limebaini kuwa kwa usafiri wa kawaida wa gari, gharama za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hazizidi shilingi 150,000.

Juzi Jeshi la Polisi kwa kutumia helikopta yake inayodaiwa kuwa na uwezo wa kubeba watu wanane, lilimsafirisha Sheikh Ponda hadi mkoani Morogoro ambako alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na kusomewa mashtaka ya uchochezi yanayomkabili.

Sheikh Ponda aliwasili kwa helikopta hiyo na kutua kwenye uwanja wa gofu, Morogoro akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na alipakiwa tena kwenye gari maalumu ambalo liliongozana na mengine matatu ya polisi kuelekea eneo la mahakamani.

Baada ya kumalizika kusomwa kwa kesi hiyo, msafara ule ule ulimrejesha uwanja wa gofu saa sita mchana na kupandishwa tena kwenye helikopta kurejea jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, gharama hizo zinazozidi shilingi milioni 10 ni zile za helikopta tu, mbali na nyingine zikiwemo posho pamoja na magari yaliyotumika kumsafirisha wakati alipotua na kurudi katika uwanja wa gofu.

MTANZANIA Jumatano limedokezwa kuwa ndani ya Jeshi la Polisi, rubani anayerusha helikopta kwa muda wa saa moja, hulipwa kuanzia shilingi 100,000.

Kwamba helikopta iliyotumika kumbeba Ponda, hubeba watu wanane kwa maana ya marubani wawili na abiria wengine sita.

Hata hivyo gazeti hili limedokezwa kuwa, kwa askari ambao wanasindikiza mahabusu kama watalala wanakokwenda, hulipwa posho na kama hawalali hawalipwi.

Katika tukio la kumsindikiza Ponda hawakulala, hivyo hawakulipwa chochote.

Wakati hayo yakijitokeza, Gazeti hili kupitia vyanzo vyake vya habari vilivyoko ndani ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa hatua ya Ponda kusafirishwa kwa helikopta ilitokana na uamuzi wa baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi hilo walioko Dar es Salaam na wale wa Morogoro.

Inaelezwa kuwa viongozi hao walifikia uamuzi huo, baada ya kudai kuwapo kwa taarifa za kiintelijensia za kuwapo kwa tishio la usalama wa nchi endapo Ponda angesafirishwa kwa njia ya kawaida.

Juzi Ponda alianza kwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kufutiwa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili, baada ya kusomewa mara ya kwanza Agosti 14 mwaka huu akiwa kitandani katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kumshitaki.

Alidaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano kati ya Juni 2 na Agosti 11 mwaka huu.

Ponda alifikishwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na baadaye alipandishwa kizimbani na kufutiwa kesi hiyo baada ya Wakili Kweka kuwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Baada ya kufutiwa mashtaka hayo, alichukuliwa na kupelekwa Morogoro ambako pia alisomewa mashtaka ya uchochezi.

WACHUNGAJI WA DESI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3, MMOJA ACHOMOKA .kisa kamili ni hv

Mchungaji Albogast baada ya kuachiwa huru.
Akikumbatiwa na mpendwa wake.
Wachungaji wengine wakirudishwa rumande kwa muda kusubiri hukumu.
Wakirudishwa rumande.
...Hapa wakati wakisubiri hukumu kizimbani.
Wakili wa washitakiwa, Atson Ndusyepo akiongea na wanahabari baada ya hukumu.
Umati wa watu wakiwemo waliokuwa wateja wa Desi waliofika mahakamani hapo kujua hatima ya fedha walizopanda wakitoka nje ya mahakama baada ya kuambiwa hawana chao.
Wachungaji watano wa makanisa ya Pentekoste waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuendesha biashara ya upatu kupitia Taasisi yao ya Desi Tanzania na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu leo mmoja wao aitwaye Albogast Francis ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia wakati wengine wanne wakihukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 21 kila mmoja pamoja na kutaifishwa mali zao.
Kesi hiyo ambayo imeunguruma kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar takribani miaka minne, kupitia kwa hakimu wake, Aloyce Katemana ilitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa utetezi na Jamhuri. Vilevile kwa wale wote waliopanda katika taasisi hiyo wote wameonekana kutenda kosa, hivyo hawana chao.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ahudhuria Swala ya Iddi el Fitri

IMG_3014 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid karume wakati wa Swala ya Idd el Fitri iliyosaliwa Kitaif
katika viwanja vya Maisara Suleiman,Mjini Unguja.[Picha na RamadhaOthmanIkulu.]IMG_3028
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ,akiswalisha Swala ya Idd el Fitri,ambayo kitaifa iliwaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja leo katika kufuatia kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3038
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala ya Idd el Fitri,iliyoswaliwaa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3042
Akina mama waumini wa Dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Idd el Fitri katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3055
 Imamu Mkuu wa Msikiti Masjid  Mushawal Mwembeshauri Sheikh Mziwanda Ng’wali Ahmed,akitoa hutuba ya swala ya idd el fitri,katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Ungujaleo katika kusherehekea sikukuu hiyo kwa wailamu wote Duniani.[Picha naRamadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3038
Baadhi ya Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi baada ya kumalizika kwa swala ya Iddi el fitri

Sikukuu ya Idd leo, Waislamu wajitafakari upya juu ya mkanganyiko uliopo usiokuwa wa lazima

   Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam LEO ni Sikukuu ya Idd el Fitr. Waislamu wote duniani na wale wasiokuwa waumini wa dini hiyo wanafurahia siku hiyo baada ya kumaliza mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakifanya ibada
Takribani siku 30 Waislamu walikuwa kwenye mfungo huo, ambao kuna kila sababu ya waumini hao kujitafakari upya. Kila siku ya Mungu, wenye imani ya dini ya Kiislamu wanatumbukia kwenye mkanganyiko wa aina yake duniani.
Kumekuwa na changamoto nyingi, hasa hili la dini moja kuwa na madhehebu lukuki, tena hata yale yasiyokuwa na tija. Naomba niwe muwazi 
Mimi ni muumini wa dini hii ya Kiislamu. Nimezaliwa katika misingi ya dini hii, hivyo lolote linaloweza kutokea tofauti, nabaki nawaza namna ya kudumisha jamii bora.
Naelewa kuwa Tanzania haina dini lakini watu wake wana dini. Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaongoza nchi isiyofungamana na dini yoyote, ila yeye mwenyewe ana dini yake.
Ni wazi tunapaswa kuthaminiana na kuheshimiana pia. Hata hivyo, ni vyema kwenye mapungufu yasemwe kwa ajili ya kujenga jamii bora na kuacha mkanganyiko huu.
Ingawa leo ndio siku ya Idd, lakini jana baadhi ya waislamu waliswali kuonyesha kuwa ndio siku sahihi. Hapa dini moja, lakini inagubikwa na mkanganyiko mkubwa.
Walioswali jana wamezingatia nini tofauti na hawa walioswali leo, yani siku ya Ijumaa? Inawezekana walioswali jana wapo sahihi, lakini ni vyema masheikhe na wanazuoni wakalitolea ufafanuzi suala hili, kwanini ibada moja inayoangaliwa kuandama kwa mwezi na kuzama inapokuwa tofauti bila sababu za msingi?
Sheikhe Mkuu wa Tanzania, Shaban Simba kwa kushirikiana na wanazuoni wengine wa dini ya Kiislamu wanapaswa kujua kuwa dini yao inapotezwa na mitazamo ya kukanganya.
Mtu anaweza kuhoji, huyu anayeswali leo na yule aliyefanya hivyo jana kuna otofauti gani wakati wote wanapaswa kufunga au kufungua kwa kuangalia kuandamana kwa mwezi.
Watu wanasema kuwa mwezi umeandama Oman, Arabun, hivyo ni wakati wao kuswali Idd. Suala hili linachanganya na kuumiza sana vichwa, maana hali hii isipoangaliwa huenda ikaharibu thamani ya Uislamu.
Mtaa mmoja malumbano mengi yanaibuka. Kila mtu anajiona yupo juu ya mwenzake. Huyu amefunga na yule amefungua. Hali hii inauma na kukera kupita kiasi.
Vyema suala hilo likaangaliwa kwa mapana yake. Kuna hatari watoto wanaozaliwa leo wakashindwa kutambua wasimame wapi.
Dini ya Uislamu inakabiriwa na changamoto nyingi na ndio maana hadi leo waumini wake wanalia kukandamizwa, wakati wenyewe wamegawanyika.
Hakuna kinachofanywa kwa ajili ya kuujenga Uislamu na ndio maana hata uwapo wa Simba Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), linachanganya kuona wengi wao hawakubaliani nalo.
Lengo si kukashifu ila kuwakumbusha watu wawe makini katika mfumo huu unaoibua maswali kedekede kwenye jamii.
Nakutakia Idd Njema mdau

"TUMECHOKA KUONGOZWA NA MAKAFIRI, LIPIZENI KISASI NA MTAPATA UHAI MZURI"....HUU NI UCHOCHEZI WA SHEIKH PONDA .

SERIKALI imenasa kanda za video zinazomuonyesha Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, akitoa mahubiri yanayowahamasisha waumini wa dini ya Kiislamu kuanzisha uasi dhidi ya serikali.

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA URU LAKUMBWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA ( UCHAWI )


HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina.
 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved