skip to main |
skip to sidebar

MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘,
Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo
atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi)
yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya
kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi
30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza
na gazeti hili hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance
alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata
kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa
kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi
alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona
kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba
wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena,
akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo
kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance
pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo
iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward
ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.

“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho.
Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni
madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani
mkweli hapo?”
Stori: Waandishi Wetu
VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya
‘Masogange’ na shosti yake, Melissa Edward wapo huru kufuatia kesi
iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika Kusini ya kukamatwa na madawa ya
kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8, lakini
baadhi ya wadau nchini wanasema kuna mchezo umechezwa, Ijumaa Wikienda
limebaini mambo ya kushangaza nyuma ya pazia.
Masogange na Melissa walikamatwa Julai
5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo
Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo. Wawili hao wameishi
mahabusu kwa saa 1824.
MMOJA HURU, MMOJA AHUKUMIWA
Uhuru wa Masogange ni baada ya Mahakama
ya Kempton jijini Johannesburg kumtia hatiani kwa kuingiza kemikali
hatari nchini humo, akatakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni
4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela.
Melissa yeye hakukutwa na hatia kwa vile
ilibainika mizigo aliyokutwa nayo aliombwa na Masogange amsaidie kubeba
baada ya kukutana ndani ya ndege ya Shirika la South Africa Airlines.
KUMBE SI CRYSTAL MATHAMPHETAMINE
Habari kutoka nchini humo zinasema
mdhamini wa Masogange (jina halijapatikana) alipigana kuhakikisha staa
huyo na nduguye ambaye amezaliwa naye kwa mama mkubwa wanakuwa huru na
kurejea Bongo.
Katika kupigana huko, mdhamini huyo
alifurahia matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa serikali ya nchi hiyo
kuyaona madawa hayo kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine
ambayo si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa
nyingine hupatikana unga halisi.
Kwa Bongo madawa hayohayo ni unga na
tayari watu wengi wapo korokoroni kwa kukamatwa nayo akiwemo aliyekuwa
rafiki wa marehemu Steven Kanumba, Saada Ally.
Katika hilo, mtu anayekamatwa na madawa
hayo nchini humo hushtakiwa kwa kosa la kuingiza kemikali hatari.
Serikali ya Afrika Kusini ilipiga marufuku kuingizwa nchini humo kwa
madawa hayo na adhabu yake iko wazi.
“Yule mdhamini alipojua mkemia mkuu
amesema yale si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine aliitumia
nafasi hiyo kucheza na mwanasheria ambapo kifungo chake kinajulikana,”
alisema mtoa habari wetu mmoja.
MSEMAJI WA ‘TRA’ YA SAUZ AINGIA SHAKA
Habari zinasema kuwa, kufuatia taarifa
za mahakama kwamba mzigo huo si Crystal Methamphetamine bali ni
Ephedrine Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini (SARS), Marika
Muller alisema kuwa timu yake ina uhakika wa asilimia mia moja kwamba,
mzigo wote wa Masogange na Melissa walioukamatwa nao ni madawa ya
kulevya aina ya Crystal Meth.
Muller akatoa la moyoni akisema kwamba,
kama mahakama imekubaliana na matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa
nchi hiyo, yeye hana la kusema kwa kuwa uamuzi wa korti ni wa mwisho.
KAMANDA NZOWA ANYOOSHA MIKONO
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kamanda wa
Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey
Nzowa ambapo alipoulizwa juzi kama serikali ina mpango wa kumkamata
Masogange atakaporejea nchini ili awataje waliomtuma, alisema:
“Sasa kama wameachiwa kule, sisi
tutawakamataje? Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kesi ilisikilizwa kule
mahakama ikafikia ilipofikia, basi tena! Ila tutafuatilia chini kwa
chini mtandao huo.”
MCHEZO UMECHEZWA
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya wasomaji
walipozungumza na gazeti hili juzi walitilia shaka kuwepo kwa mazingira
ya kuchakachuliwa kwa madawa hayo.
Walisema kuwa, ilikuwaje SARS iwakamate
akina Masogange na kugundua walibeba Crystal Meth (unga) halafu mahakama
iseme ni Ephedrine (kemikali hatari)?
“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho.
Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni
madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani
mkweli hapo?” alihoji msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Aunt
Elizabeth, mkazi wa Mbezi Beach, Dar.
Wengine walitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter wakidai hivyohivyo kwamba kuna mchezo umechezwa.
“Kwanza wamekamatwa Julai 5, mwaka huu.
Kesi imeisha katikati ya wiki iliyopita, hata miezi mitatu haikufika.
Hapa Bongo, yule mama Leila (Mwanaidi Mfundo) na wenzake walikamatwa
2011 kwa unga huohuo, kesi yao bado ipo Mahakama Kuu, Dar hadi leo,”
alisema Samuel Msalanda wa Ilala, Dar.
Wengi walionesha kutilia shaka hukumu
hiyo kutokana na mitazamo yao lakini Mahakama ya Kempton jijini
Johannesburg, Afrika Kusini ndivyo ilivyoamua.
MASWALI TATA
Ukiachana na mitazamo na ukweli ulivyo,
bado kuna maswali tata ambayo utatuzi wake unakuwa mgumu kulingana na
kesi yenyewe kuanzia kutajwa, kusikilizwa hadi hukumu ilikuwa nje ya
Tanzania.
Je, mwenyewe Masogange alipokuwa akisafirisha dawa hizo alijua ni kemikali hatari ambayo ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?
Iwe ni kemikali au la! Alitoa wapi mali ghafi hiyo na alikuwa akimpelekea nani kule Afrika Kusini?
Ni kigogo au mtu gani aliyeratibu safari hiyo mpaka Masogange akafanikiwa kupita kwenda Afrika Kusini?
Nani alimpeleka Masogange hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)?
Kituo cha kwanza cha Masogange kuondokea
kwenda JNIA kilikuwa wapi? Inawezekana ni nyumbani kwake ambapo alilala
na mizigo yote ile?
Kama mahakama imebaini Masogange
hakuingia Afrika Kusini na unga, vipi kuhusu wale wafanyakazi wa JNIA
walioachishwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kwa
kuzembea Masogange akapita na ule mzigo?
Yupo wapi Nassoro Mangunga aliyetajwa na Dk. Mwakyembe kuwa alifanikiwa kutoroka na mabegi matatu ya unga kule Sauzi?
Source:Global Publishers
Support :
Copyright © 2011.
HABARILINE - All Rights Reserved