Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa
Mkapa aliyasema hayo mjini hapa katika
mahafari ya kwanza ya Chuo kikuu cha Askofu Mihayo Tabora (AMUCTA ),
chuo kishiriki cha mtakatifu Agostino yalifanyika kwenye viwanja vya
chuo hicho mjini Tabora.
Alisema kuwa anahisi jamii kwa sasa ina
ari ya kutafuta majibu ya matatizo na changamoto zinazowakabili na
kutokana na njaa kubwa ya maendeleo inapendelea kudakia kupata majibu ya
haraka haraka kama vile matangazo ya biashara katika radio na runinga,
badala ya kuwa tayari kuonesha utayari wa kutumiza wajibu.
Alisema matokeo yake ni malalamiko
yasiyoisha na kusahau kwamba subira yavuta heri, na kuongeza kuwa kiini
cha matatizo kinapaswa kichunguzwe kwa makini na changamoto ya elimu
inavyoweza kukabiliwa.
Alisema kwa njia hiyo wigo wa fikra
utapanuliwa na kuweka misingi imara zaidi ya kutatua matatizo
yanayozunguka jamii hasa elimu na miundombinu mbalimbali.
Awali mkuu wa chuo cha AMUCTA, Padre Dk.
Javenalis Asantemungu, alisema chuo hicho, kilianza rasmi Novemba 2010
kikiwa na wanafunzi 885, ambapo 51 waliahilisha masomo kutokana na
sababu mbalimbali wawili walifariki dunia, 116 wamesoma hadi mwisho
lakini hawakutimiza vigezo vya kuhitimu. Wahitimu wa jana walikuwa 718.
Padre Asantemungui aliwataka wakazi wa
mkoa wa Tabora ambao hawawezi kujiunga na masomo ya asubuhi na mchana
chuo kinaendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili kwa muda wa jioni,
utaratibu huo umeanza kuitikiwa na watumishi mbalimbali wa serikali na
sekta binafsi.
SOURCE:
NIPASHE JUMAPILI