Msanii wa kike wa filamu bongo maarufu kwa jina la Husna Chobis ‘Avana’ amedai kuwa yeye hataki kuwa na mwanaume wa kibongo kwa sababu wengi wao ni waongo na hawayajui mapenzi...
Akiongea na mwandishi wetu, mrembo huyo alidai kuwa umaarufu wake humpa wakati mgumu sana wa kumtambua mwanaume mkweli maana wengi humtamani kimapenzi kutokana na jina lake ( ustaa wake )
“Sitaki kuzalishwa wala kuwa na uhusiano wa kudumu na mwanaume toka Tanzania maana wengi wao ni tapeli na hata ukiwakubali huwa hawajui kitu .
"Bora kwa nchi za wenzetu kuna ndoa za mikataba kiasi kwamba mtu unakuwa unajua kabisa nitakuwa na huyu kaka kwa muda fulani , ntazaa naye au ni wa raha tu.
"Hiyo inasaidia sana kwa sababu kama huyo kaka ni MSHAMBA inakuwa ni rahisi kwako kumpiga chini na kuangalia ustaarabu mwingine”..alisema Avana.