Mama mwenye hasira wa mmoja wa wasichana wa Uingereza waliomwagiwa
acid mjini Zanzibar ameungana na bintiye nchini humo baada ya jana
kuwasili kwa ndege kwenye hospitali kwaajili ya matibabu.
Katie Gee, aliyefunikwa blanket, na rafiki yake Kirstie Trup
wakiwasili kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster nchini Uingereza
kutibiwa majeraha yao
Mama huyo, Nicky Gee alionekana kushindwa kujizuia kulia baada ya
kumuona binti yake Katie na rafiki yake Kirstie Trup wakishuka kwenye
ambulance akiwa amefunikwa blanket.
Wasichana hao ambao wote wana miaka 18 walipelekwa kwenye hospitali
ya Chelsea and Westminster kutibiwa haraka majeraha ambayo baba yake
Katie ameyaita mabaya yasiyoelezeka.
Wote wameungua vibaya baada ya kumwagiwa tindikali usoni wakati
walipokuwa wakiingia kwenye mgahawa mjini Zanzibar.
Hilo lilikuwa
shambulizi la tatu wakati walipokuwa visiwani humo. Awali mmoja wa
wasichana hao alishambuliwa na msichana wa kiislam baada ya kumsika
akiimba wimbo wakati wa mwezi wa Ramadhan.
Katie na Kirstie
Polisi wamedai kuwa washukiwa saba akiwemo muongozaji wa watalii
wamekamatwa jana asubuhi.Na sasa zawadi ya paundi £4,000 imetangazwa
kutolewa na polisi Zanzibar kwa atakayesaidia kupatikana kwa kwa
wahalifu hao.
Marafiki wanadai kuwa walikuwa wamelengwa kushambuliwa kwasababu
walikuwa ni wayahudi na polisi wanadai kuwa walikuwa wanataka kuongea na
mhubiri wa kiislam ambaye huenda ndiye alipanga shambulizi hilo.
Polisi
wamedai kutoa warrant ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda Issa, ambaye
inasemekana mafundisho yake yamechochea mashambulizi hayo ya tindikali.
Wasichana hao watapata matibabu ya kina kutokana na mejeraha
waliyoyapata kwa kumwagiwa tindikali hiyo iliyomwagika usoni, kifuani,
miguuni na mgongoni.
Katie
Mikono yao pia imejeruhiwa kwakuwa walikuwa wakijaribu kufuta
tindikali hiyo. Baba yake na Miss Trup, Marc, 51, milionea na daktari wa
meno alisema mpita njia alienda kuwasaidia wasichana hao baada ya
kushambuliwa na alimpigia simu.
Marafiki hao walikuwa wameenda Zanzibar kama walimu wa kujitolea kwenye kituo cha watoto yatima. Tukio hilo linaweza kuathiri vibaya sekta ya utalii visiwani Zanzibar.
TOA MAONI YAKO HAPA