MSANII wa maigizo Bongo, Steve Mangere ‘Steve Nyerere’ amefunguka
kuwa mkono wake umepona lakini hakupata tiba kwa mganga wa kienyeji
kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Akichezesha
taya na Stori 3, Steve alisema mkono wake umepona kwa njia za kawaida
kabisa na anawashukuru wote waliomfariji alipokuwa akiumwa. “Nimepona mkono wangu, lakini sijatibiwa kwa mganga kama watu wanavyodai. Nimepona tu kwa njia za kawaida. Nawashukuru wote waliokuwa wakinijulia hali,” alisema msanii huyo mkongwe.