Wapendwa wana CCM, itakumbukwa mnamo tarehe June 3, 2013 Tume ilitangaza Rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hatua hii ya mwanzo ya kukamilika kwa katiba mpya ni sehemu ya kwanza ya
kukamilika kwa katiba. Pia, ikumbukwe hatua ya pili ni kuwasilishwa
rasimu ya pili kwenye Bunge la Katiba. Mwisho, kutakuwa na Rasimu ya
tatu itakayofikishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Wana CCM, hatua hii ya pili ya tume ya katiba ni kwamba inajadiliwa
katika mfumo wa mabaraza ya asasi na vyama vya siasa. Kwa kuzingatia
kwamba chama cha mapinduzi ni taasisi muhimu na yenye maslahi makubwa
katika upatikanaji wa katiba mpya.
Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ilikutana mjini Dodoma tarehe
October 6,2013 ilitoa maamuzi ya kwamba uandaliwe ufafanuzi
utakaorahisisha utoaji wa maoni utakaotumiwa na wana ccm katika kutoa
maoni.
Madhumuin ya mpango huu ni kuwawezesha wana CCM kushiriki na kutoa maoni yao kikamilifu kutoka ngazi ya matawi hadi Taifa.