Home » » Ifahamu Shule isiyojua ladha ya dawati kwa miaka 40

Ifahamu Shule isiyojua ladha ya dawati kwa miaka 40

Darasa linalotumika kufundishia wanafunzi, likiwa halina dawati hata moja jambo linalosadikiwa kuwa wanafunzi wanakaa juu ya mawe 
******
Simiyu. Kwa wengi taarifa za ukosefu wa madawati kwenye shule za umma na haswa zile za msingi, siyo za kushangaza. Tumezoea kusikia shule ikiwa na upungufu wa madawati kadhaa lakini siyo kutokuwa na dawati kabisa kwa miaka takribani 40.
Shule ya Msingi ya Mwaswale iliyopo Tarafa ya Bumela Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, ina historia ndefu ya ukosefu wa madawati kwa kipindi cha miaka 40 sasa.
Tatizo hilo limekuwa ni kero ya muda mrefu hali inayowafanya wanafunzi na walimu wake kukata tamaa ya kuendelea na masomo katika shule hiyo.
Mwaswale ina wanafunzi 1,268 ambao wanalazimika kuketi kwenye mawe kwa sababu ya ukosefu wa madawati.
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1973 ikiwa madawati 80, baada ya muda mfupi yaliharibika na kuifanya kubaki kama makumbusho kutokana na wanafunzi wake kukalia mawe au matofali.

Mwandishi wa makala hii alipofika shuleni hapo, alishuhudia wakiwa wameketi kwenye mawe na matofali yaliyopangwa katika mstari na kuleta mtiririko.
Baadhi ya wanafunzi wanasema hali hiyo inatokana na wazazi wao kutoshiriki kuchangia maendeleo ya elimu huku wengine wakiilaumu serikali kwa kushindwa kufuatilia hiyo.
Steven Kwabi anasema licha ya familia nyingi kujihusisha na kilimo wilayani humo, wazazi hawana mwamko katika suala la maendeleo ya elimu.
Mwanafunzi huyo anaiomba serikali na wadau wengine kuwasaidia kupata madawati hali itakayowasaidia kuwaepusha na magonjwa yatokanayo na vumbi.
“Tukipata madawati tutaepuka magonjwa kama mafua na hata kifua kikuu, pia itatusaidia kuandika vizuri tofauti na sasa tunavyoandikia kwenye magoti,” aliongeza.
“Wazazi hawataki hata kuchangia Sh100 za huduma ya uji kwa miezi sita, akiulizwa anasema mbona shule ya jirani hawanywi uji,” anasema Kwabi.
Naye Mabula Masunga anayesoma darasa la tano shuleni hapo, atajisikia vizuri kama shule yake itasaidiwa madawati ili nao wasome kwa furaha kama watoto wa shule nyingine

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved