Maisha Tuck Shop lililopo Barabara ya Veld, Athlone, ambapo Watanzania watatu walipigwa risasi na kufariki.
Watanzania watatu waliuawa Jumanne
iliyopita jijini
Cape Town, Afrika ya Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya
madawa ya kulevya. Watanzania hao walipigwa risasi na kundi la watu
waliokuwa wameficha nyuso zao nje ya duka lijulikano kama Maisha Tuck
Shop lililopo katika barabara ya Veld katika kitongoji cha Athlone,
jijini Cape Town.
Watanzania
wawili walifariki hapo hapo na mmoja alifariki baada ya kufikishwa
hosipitali. Mwanamke mmoja, raia wa Afrika Kusini, alijeruhiwa vibaya
katika shambulio hilo. Mmiliki wa duka hilo, Ashim Nassoro, alisema kuwa
aliona kundi la watu wakiwa na bunduki za aina ya AK-47 na pistols
wakipiga risasi nje ya duka lake.
Bw.
Nassoro alisema amesikitika sana na shambulio tukio hilo na kudai
waliouawa walikuwa marafiki zake. Alisema yeye alikuwa ndani ya nyumba,
ambayo iko karibu na duka hilo pamoja na mke wake na mtoto wake wa miaka
mitatu wakati milio ya risasi ilipoanza.
“Nilikuwa
ndani na nilimwambia mke na mtoto wangu walale chini mpaka milio ya
risasi iishe” alisema Nassoro na kuongeza “waliwapiga risasi watu
waliokuwa ndani ya nyumba halafu wakaenda kwenye duka. Walikuwapiga
risasi watu wawili dukani, mmoja aliyekuwa kwenye geti na mwanamke mmoja
aliyekuwa kwenye nyumba.”
Nasoro
aliongeza kuwa alikuwa anawajuwa Watanzania hao kwa sababu wote
wanatoka Tanzania na wamekuwa wakiishi pamoja tokea walipowasili Cape
Town miaka mitano iliyopita. Mtu mwingine aliyeshughudia tukio hilo
alisema kuwa waliowauwa Watanzania hao walikuwa hawana wasiwasi na
walirudi kwenye gari yao taratibu na kuondoka eneo la tukio.
Kufuatia
tukio hilo, polisi ilimkamata Abdus Salaam Ebrahim ambaye ni kiongozi
wa kikundi kinachopiga vita dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya nchini
humo kinachojulikana kama People Against Gangsterism and Drugs (Pagad).
Abdus Salaam Ebrahim amefikishwa mahakami leo kwa mashtaka ya mauaji.
Hata
hivyo, mahakama imeyaondoa mashtaka hayo kwa muda kufuatia ombi la
mwendesha mashtaka ili kuruhusu uchunguzi zaidi kufanyika. Wakati hakimu
akiyandoa mashtaka hayo, wafuasi wa kikundi hicho cha Pagad waliokuwa
wamejazana mahakamani hapo walishangilia huku wakisema “Allahu Akbar”.
Majina ya Watanzania waliouawa hayakuwekwa kwenye charge sheet.
Pagad
ni kikundi kilichoanziswa mwaka 1995 kupambana na uhalifu na madawa ya
kulevya kwenye jiji la Cape Town baada baada ya juhudi za serikali
kulegalega. Kampeni ya kikundi hiki ilianza mwaka 1996 baada kumkamata,
kumpiga na kumchoma moto hadi kufa Rashaad Staggie ambaye alikuwa
kiongozi wa kikundi cha uhalifu jijini Cape Town. Serikali ya Afrika
Kusini ilishawahi kudai huko nyuma kuwa Pagad ni kikundi cha kigaidi
baada ya kudaiwa kulipua kwa bomu hoteli ya Planet Hollywood mwaka 1998.
Hata hivyo, Pagad ilipinga kuhusika kwenye shambulio hilo.
Kikundi
hiki kilipotea lakini kikaja kuibuka tena kuanzia mwaka 2011 na kampeni
yake ya kuchukua mitaa inayotawaliwa na uhalifu na biashara ya madawa
ya kulevya. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa kurudi tena kwa Pagad kwa gia
ya kupambana na uhalifu, hasa madawa ya kulevya, itafanya hali kuwa
mbaya hasa kwenye jimbo la Western Cape.
Hivi
karibuni kumekuwa na ongezeko la milipuko ya mabomu kwenye sehemu
zinazouza magari na pia kwenye nyumba za makazi ya watu zilizopo Athlone
na maeneo mengine jijini Cape Town. Matukio haya yamekuwa yakitokea
zaidi kwenye nyuma za makazi zinazotuhumiwa kutumika kufanyia biashara
ya madawa ya kulevya. Kikundi cha Pagad kimekanusha kujihusisha na
matukio hayo.
Source:- JF Blog