Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni aliingia mzigoni kutengeneza filamu
na staa kutoka Ghana, Van Vicker, anasema lugha ina mchango mkubwa
katika mafanikio ya filamu.
Mbali ya hilo, Irene ametumia wasaa aliopewa na gazeti hili kuwaasa
Watanzania wakiwamo wasanii wenzake kwamba wawekeze kwenye suala la
elimu la hususani lugha ya Kiingereza akisema ndiyo kikwazo kimojawapo
kwa baadhi ya vijana kutopata ajira.
IRENE Paul, staa aliyewahi kutamba katika filamu za Kalunde, Saturday
Morning, Kibajaji, Love & Power, Handsome wa Kijiji na nyinginezo
nyingi, amesema ndoto ya filamu za Tanzania kutamba Afrika haitatimia
kama waigizaji wake wataendelea kutumia lugha ya Kiswahili tu.
Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni aliingia mzigoni kutengeneza filamu
na staa kutoka Ghana, Van Vicker, anasema lugha ina mchango mkubwa
katika mafanikio ya filamu.
“Sitaki kusema watu waache kuigiza filamu za Kiswahili, ninajua kwamba
tuna wateja wengi Bongo na pia ni wajibu wetu kuhakikisha lugha yetu
inakua,” alisema.
“Lakini hatupaswi kuufumbia macho ukweli kuwa Kiingereza ndio lugha itakayotupaisha kimataifa.”
Mbali ya hilo, Irene ametumia wasaa aliopewa na gazeti hili kuwaasa
Watanzania wakiwamo wasanii wenzake kwamba wawekeze kwenye suala la
elimu la hususani lugha ya Kiingereza akisema ndiyo kikwazo kimojawapo
kwa baadhi ya vijana kutopata ajira.
“Sasa hivi baadhi ya ofisi zetu zimetawaliwa na watu kutoka nchi za
jirani, hata sisi wasanii baadhi yetu tunashindwa kuvuka mipaka huku
lugha hiyo (Kiingereza) ikiwa ni kikwazo,” anasema na kuongeza.
“Ni wakati wetu Watanzania kujikita katika suala hili, pia hata kwa
wasanii wenzangu. Wenzetu wa Nigeria, Ghana na kwingineko wanatamani
kufanya kazi na sisi, lakini wakijaribu kuangalia filamu zetu na lugha
tunayoitumia wanapata wakati mgumu japokuwa ni lugha ya taifa.”
Akizungumzia suala la waigizaji kugeukia kazi ya kuongoza filamu, Irene,
anasema kwamba kamwe hawezi kuwa mwongozaji wa filamu kama ilivyo kwa
wasanii wengi wenye majina, badala yake kazi hiyo anawaachia watu
wengine ili kila kazi anayoifanya iwe na umakini na utaalamu zaidi.
Kuna tabia imejengeka kwa baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo kujivika
madaraka mengi yakiwamo ya mwongozaji, mtayarishaji na mwigizaji katika
filamu moja.
Anasema hali hiyo inasababisha umakini katika utayarishaji wa filamu kupungua.
“Mimi nimeamua kuwa chachu ya mabadiliko, nimeona bora nimuite mtaalamu
wa kuongoza afanye kazi yake, mtayarishaji naye afanye kazi yake ili
mwisho wa siku, macho na mawazo ya wengi yaweze kuzaa kitu ambacho
kitasaidia kusukuma ubora wa kazi zetu,” alisema.