THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hakuna uporaji wa ardhi ya wakulima wadogo unaofanywa na Serikali – JK
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa hakuna uporaji wowote wa ardhi unaofanywa na Serikali yake
dhidi ya ardhi ya wananchi na hasa wakulima wadogo.
Aidha,
Rais Kikwete amesema Serikali ya Tanzania haiwezi kupora ardhi ya
wananchi na hasa wakulima wadogo kwa sababu sera za kilimo za Serikali
zinalenga kumlinda mkulima mdogo na kumwezesha kujikomboa kutoka kwenye
umasikini.
Rais
Kikwete alitoa msimamo huo, kwa mara nyingine tena, mwishoni mwa wiki
wakati alipozungumza na wana-jumuia ya Chuo Kikuu cha Guelph cha
Toronto, baada ya kuwa ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya
Sheria na Chuo hicho maarufu cha Canada.
Katika
hotuba yake ya kupokea na kukubali shahada hiyo, Rais Kikwete ambaye
alizungumzia maendeleo na changamoto za kilimo katika Afrika alisema
kuwa kamwe Serikali ya Tanzania haiwezi kupora ardhi ya wakulima wadogo
wadogo kwa sababu sera ya
Serikali katika mipango yote mikubwa ya kilimo ni kumlinda na kumtetea mkulima mdogo.
Serikali katika mipango yote mikubwa ya kilimo ni kumlinda na kumtetea mkulima mdogo.
“Hakuna
uporaji wa ardhi unaofanywa na Serikali katika Tanzania kama
inavyodaiwa na baadhi ya watu. Uporaji wa ardhi ya mkulima mdogo hauwezi
kutokea katika Tanzania kwa sababu sera za Serikali ni kuhakikisha kuwa
mkulima mdogo anakuwa mtu wa kwanza kunufaika na kufaidika na sera za
kilimo za Serikali,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mkulima
mdogo yuko katikati ya mipango na sera za Serikali, na kwa kweli ndiye
mtu muhimu zaidi katika mipango ya kilimo ya Serikali. Kazi ya wakulima
wakubwa ambao tunawakaribisha kuwekeza katika Tanzania ni kuunga mkono
shughuli za kilimo za wakulima wadogo kwa maana kweli kweli ya
uwezeshaji.”
Rais
Kikwete amesema kuwa kwa kadri Serikali inavyokaribisha wakulima
wakubwa kuwekeza katika kilimo na uchumi wa Tanzania, ni dhahiri kuwa
Serikali itaendelea kuwalinda na kuwatetea wakulima wadogo ambao
watashirikiana na wakulima wakubwa katika kuboresha kilimo cha Tanzania.