Home » , , , » MTUHUMIWA AJINYEA MAHAKAMANI WAKATI AKISOMEWA KIFUNGO CHA MIEZI 6 JELA JIJINI DAR...

MTUHUMIWA AJINYEA MAHAKAMANI WAKATI AKISOMEWA KIFUNGO CHA MIEZI 6 JELA JIJINI DAR...


 
 
Mtu mmoja amehukumiwa kifungu cha miezi sita jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive kwa kosa la kujisaidia haja kubwa ndani ya Mahakama wakati akisomewa mashitaka. 

Adhabu hiyo ilitolewa papo hapo baada ya mshitakiwa Hassan Omary (25) kufanya kitendo hicho aliposomewa mashitaka mengine tofauti.
 
Hakimu William Mutaki ndiye aliyetoa hukumu hiyo. Wakati akisomewa mashitaka sanjari na washitakiwa wengine watatu ya kubughudhi abiria maeneo ya Kariakoo, Omary inadaiwa alitokwa haja kubwa.
 
Mwandishi alishuhudia mshitakiwa huyo akisafisha eneo la mahakamani alikochafua kabla ya kupelekwa jela. Wengine anaoshitakiwa nao katika kesi hiyo ni Mohamedi Mussa (20),Hassani Ramadhani (18),Shukuru Adison (26) na Ally Omary (28).

Mwendesha mashitaka wa serikali John kijumbe alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi William Mutaki kuwa washitakiwa walitenda kosa la kuwanyanyasa na kuwabugudhi abiria ,Septemba 18 ,mwaka huu Kariakoo, jijini Dar es Salaam. Washitakiwa wengine walirudishwa rumande hadi Oktoba 2,mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
Katika kesi nyingine, mshitakiwa Jacob Sasita (28) amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja baada ya kukiri kuwanyanyasa abiria .
 
Sasita alikuwa miongoni mwa washitakiwa saba waliofikishwa mahakamani kwa kosa hilo. Washitakiwa wengine ni Ramadhani Juma (38),Abeid Ismail (25),Abuu Rajabu(25),Salimu Kijimbo (39),Ally Hassani (28),Josephb Chambo (29)na Fabiani Thomas (28) ambao walikana kutenda kosa baada ya kusomewa mashitaka.
 
Mbele ya Hakimu Mkazi Timoth Lyon, Mwendesha Mashitaka wa Serikari, Richard Magudi alidai watu hao walitenda kosa la kuwanyanyasa abiria katika kituo kikuu cha mabasai cha Ubungo ,kabla ya kukamatwa na askari polisi. Walirudishwa rumande hadi Oktoba 2 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved