Home » , » SUMAYE AIONGELEA HOJA YA MGOMBEA BINAFSI KWA MAPANA ZAIDI.nikama hivi

SUMAYE AIONGELEA HOJA YA MGOMBEA BINAFSI KWA MAPANA ZAIDI.nikama hivi


079 59f78Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amekosoa uteuzi wa kugombea nafasi za viongozi kupitia ndani ya vyama vya siasa kwa madai kuwa unachangia kuenea kwa vitendo vya utoaji rushwa. (HM)
Alisema kuwepo kwa mgombea binafsi ni njia pekee ya kudhibiti rushwa kwenye uchaguzi. "Ninaungana na mapendekezo ya rasimu ya kwanza ya katiba kwamba kutakuwepo na mgombea binafsi, kwani ninaamini hiyo ndiyo njia pekee ya kudhibiti rushwa kwenye uchaguzi."
 
Sumaye aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano la Baraza la Katiba lililoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta).
 

Alifafanua kwamba mgombea binafsi hawezi kutoa rushwa kwa wananchi wote, lakini jambo hilo linaweaza kufanyika kupitia vyama vya siasa. Wajumbe au wanachama wanaweza kupewa rushwa ili kumchagua mgombea fulani kuwania nafasi anayoitaka.
 

Hata uwe na fedha kiasi gani, ukiwa unataka kuwania nafasi ya uongozi wewe binafsi huwezi kutoa rushwa kwa wananchi wote, lakini jambo hilo linawezekana kupitia ndani ya vyama vya siasa, hivyo ninaunga mkono uwepo wa mgombea binafsi," alisema Sumaye. Mbali na maoni yake kuhusu mgombea binafsi amesema ili kuhakikisha vitendo vya ufisadi, rushwa na biashara ya dawa za kulevya zinashughulikiwa kikamlifu Katiba ijayo iunde mahakama maalumu ya kushughulikia makosa hayo.

 
Pia, Sumaye alisema hakuna haja ya kujadili muundo wa Muungano wa kuwa na Serikali tatu, kwani Serikali mbili zilizopo zinatosha na kwamba kitu cha msingi ni kutafuta njia sahihi ya kutatua migogoro iliyopo.
 

"Nafahamu kuwa Ibara ya 22 na 47 zinataja mambo ya msingi ya haki za wananchi, lakini mambo hayo yametajwa juu juu, kwani kuna vitu ambavyo vingepaswa kutolewa ufafanuzi wa kina," alisema Sumaye na kuongeza:
"Kwa sasa nchi imegubikwa na suala kubwa la vitendo vya ufisadi, rushwa, uhujumu uchumi na biashara ya dawa za kulevya jambo ambalo linachangia kuwaangamiza vijana."
 

Aidha, alibainisha kuwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo ni vyema Katiba Mpya ikaunda mahakama maalumu ili kutoa adhabu kwa watu watakaobainika kuhusika na makosa hayo. Chanzo: mwananchi

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Support : Copyright © 2011. HABARILINE - All Rights Reserved