WATU wanne wa familia moja wamefariki na wengine 13 wamelazwa hospitalini kutokana na
kula chakula chenye sumu wakati wa sikukuu ya Idi el Fitri.Watu hao
wamelazwa Kituo
cha Afya cha Lusewa wilayani Namtumbo na
Hospitali yaSerikali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO).
Kamanda wa Polisi Mkoa Deusidebit
Nsimeki, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 7:00.
Kamanda Nsimeki,alisema siku hiyo kabla ya tukio, Salum Mumba, alinunua
samaki
aliyepeleka nyumbani kwa ajili ya sikukuu ya Idi.Kamanda Nsimeki
alisema katika tukio hilo Polisi wanamshikilia mtu mmoja ambaye hakutaka
kumtaja jina ambaye atasaidia polisi
kwenye upelelezi wake. Alisema baada ya kula chakula hicho,
haikuchukua muda mrefu mtoto
alianza kuumwa naye baadaye alifariki dunia. Baadaye watoto wawili walianza kuumwa na
kufariki. Watu wengine 13 walianza kuumwa baadaye majirani walipata
taarifa na kuwakimbiza watu hao hospitali. Aliwataja waliolazwa
katika kituo cha afya cha Lusewa kuwa ni Tazamio Mumba, Zidani Mumba,
Ramadhani Mumba na Zahara Mumba wote wakazi wa kitongoji Tulieni B. Waliolazwa
katika hospitali ya Mkoa wa Songea kuwa ni Gairi
Mumba, Zamoni Mumba, Fatuma Rashidi, Samidu Mumba, Asha Omary na Sharifa Mumba. Kwa
upande wake Mganga Mfawidhi ya Hospitali ya Mkoa Songea Dkt. Benedictor Ngaiza
alisema wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo hali zao zinaendelea vizuri.