Your text goes here...
Binti aliyebakwa akiwa na mtoto aliyelawitiwa.
MWANAUME aliyefahamika kwa jina moja la Mohammed, mkazi wa Kigamboni
jijini Dar amedaiwa kuwafanyia unyama watoto wawili, akimlawiti mwanaye
wa kufikia na kumbaka mdogo wa mkewe...
Akizungumza na mwandishi wetu juzi nyumbani kwake, mke wa mtuhumiwa
huyo, Zubeda alisema watoto waliofanyiwa hivyo ni mwanaye wa kiume (6)
na mdogo wake wa kike (16) (majina tunayo).
Mwanamke huyo alisema: Nilikutana na Mohammed nikiwa na mtoto huyo wa
kiume, ndani ya uhusiano wetu tukajaliwa kupata mtoto wa kiume hivi
karibuni, hapo ndipo matatizo yalipoanza.
“Alihama chumba ili mimi nilale na kichanga, akaenda kulala na mtoto
huyo. Niliamini angemchukulia kama mwanaye kwa kuwa tulishaoana.
Baadhi ya majirani wakiwa na huzuni
“Mwaka jana alikuja mdogo wangu, tukabadili kulala, tuliwaacha watoto
hao walale chumba kimoja mume wangu akarudi chumbani. Alizua tabia ya
kutoka usiku eti kuvuta sigara kumbe alikuwa anakwenda kumwingilia mdogo
wangu,” alizidi kudai mwanamke huyo.
Alidai kuwa ikafika wakati akagundua mwanaye huyo anajisaidia kwenye
nguo na kinyesi kinakuwa na damu, akawa anampiga na kumwamuru afue nguo
mwenyewe.
“Juzi shoga yangu mmoja alikuja akaniambia amemsikia mume wangu akitamba baa kwamba amemtoa ‘usichana’ mdogo wangu.
“Nilimuuliza mtoto wangu ambapo aliniambia ni kweli baba yake amekuwa akienda chumbani kwao na kumfanyia mchezo mbaya.
“Ukweli taarifa hizo zilinishtua sana, sikutarajia mdogo wangu kama angeweza kulala na mume wangu, nilimpiga sana.
“Wakati namwadhibu mtoto wangu naye akaona kumbe kitendo kile ni kibaya
akasema hata yeye baba yake amekuwa akimfanyia mchezo mchafu kila siku
usiku,” alisema mama huyo huku akilia.
Wakati watoto hao wakikiri kufanyiwa hivyo, Mohammed alikuwa akiwasikia
na kujitetea kwamba walikuwa wakimsingizia, ghafla alipokea simu na
kusema anakwenda kwenye biashara akirudi watazungumzia suala hilo lakini
hakurudi tena.
Baada ya kuona hivyo, mke huyo alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha
Polisi cha Kigamboni na kufungua kesi mbili zenye namba KGD/RB/5218/2013
KUBAKA na KGD/RB/5244/2013 KULAWITI, mpaka sasa mtuhumiwa huyo anasakwa
na polisi.
Mwanamke huyo alisema alipewa PF3 na kuwapeleka waathirika hao Hospitali
ya Vijibweni na vipimo vilionesha waliharibiwa sehemu zao za siri.
Mama huyo alisema daktari amemwambia mtoto wake wa kiume angeweza kupoteza uhai kama angeendelea kufanyiwa mchezo huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mwema, Mwinyi Baishe alithibitisha kusikia madai hayo.
-GPL
Your text goes here...